Monday, 8 August 2016

NEW FASHION:ASYA IDAROUS KHAMINI AFANYA KWELI DALLAS, TEXAS NCHINI MAREKANI

Mamaa wa mitindo Asya Idarous Khamsini akipata picha ya kumbukumbu baada ya siku ya Jumamosi Aug 6, 2016 kufanya kweli kwenye kenya Women Reunion iliyoyanyika katika hotel ya Hilton Garden Inn  iliyopo mtaa wa State Highway Dallas, Texas nchini Marekani.
Mlimbwende wa mitindo akiwa kwenye kivazi kilichowavutia wengi kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini alipofanya kweli siku ya Jumamosi Aug 6, 2016  kwenye kenya Women Reunion iliyoyanyika katika hotel ya  Hilton Garden Inn  iliyopo mtaa wa State Highway Dallas, Texas nchini Marekani.
Mlimbwende akiwa katika pozi na kivazi cha mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
Ni Kivazi kingine kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
Mlimbwende katika picha.
Mlibwende katika picha akiwa na kivazi kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
Asya Idarous Khamsini ni Balaa tupu.
Mlimbwende akiwa ametokelezea kweli na kivazi kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
Picha ya pamoja.

NEW AGRICULTURE BANK:Benki ya Kilimo yapanga kutoa huduma nchi nzima

Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza na wanahabari wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto) akizungumza na wanahabari wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi. Kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Wapili Kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ndg. Godfrey Weston Zambi (Wapili Kulia) wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi. Wengine pichani ni viongozi waandamizi wa TADB wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kushoto).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka (Wapili Kulia), akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Wapili Kushoto). Wengine pichani ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) na Bw. Adam Kamanda (Kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Kushoto) akipata maelezo kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kulia).
Afisa wa TADB, Bw. Victor Mziray (Kulia) akiwahudumia wateja waliojitokeza kutembelea Banda la Benki ya Kilimo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) akimsikiliza Bibi Constancia Mahanga (Kushoto) wa Kikundi Umoja kutoka Tandahimba wanaodhaminiwa na TADB.
Afisa Masoko wa Wakala wa Mbegu, Bi. Jacqueline Itatiro (Kushoto) akimuelezea namna ya Wakala huo unavyofanya kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia). Wengine pichani ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Wapili Kulia) na viongozi wengine wa Benki hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) akiangalia unga wa muhogo unaozalishwa na Kikundi cha Vijana cha Agripreneur. Kushoto wanakikundi wa kikundi hicho, Bw. Fortunata Mwananjela na Bi. Veronica Kichanta.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Katikati) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Wapili kulia) wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Wakulima cha Nzihi, Bw. Emmanuel Fungo anayewakilisha vikundi nane (8) vya mkoa wa Iringa waliopatiwa mkopo na TADB.


Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imepanga kuanza kutoa mikopo kwa wakulima wadogo na wakulima wakubwa wanaosaidia wakulima wadogo nchi nzima ili kuharakisha mapinduzi ya kilimo nchini.

Mikakati hiyo iliwekwa bayana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi.

Bibi Kurwijila alisema kuwa TADB inalenga kutelekeza kwa vitendo Maelekezo ya Serikali ya kupunguza changamoto zinazowakabili wakulima nchi kote, hivyo TADB imejipanga kuwafikia wakulima wadogo nchi nzima ili kuharakisha mapinduzi ya kilimo nchini.

“Benki imejipanga kutoa mikopo yenye riba nafuu katika muda mfupi, wa kati na mrefu kwa Wakulima wadogo wadogo, wa kati na wakubwa, hususan kuziba pengo la upatikanaji wa fedha za kwenye mnyororo wa ongezeko la thamani ili kuharakisha mapinduzi ya kilimo katika tasnia za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu (ufugaji nyuki),” alisema Bibi Kurwijila.

Aliongeza kuwa kwa sasa Benki imeanza kupokea maombi kutoka kwa wakulima wanaohitaji mikopo nchi nzima ili kuwakwamua na changamoto ya ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini.

Akizungumza katika Maonesho hayo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi alisema kwamba Benki yake imetimiza mwaka mmoja kwa kutengeneza faida kwa kupata jumla ya kiasi cha Shilingi 450 milioni kwa mwaka jana na Shilingi 1.72 bilioni kwa miezi sita (6) ya mwaka 2016.

“Benki imeanza kazi kwa kishindo kwa kutengeneza faida jambo linaloonyesha uimara wa Benki katika kuwahudumia wakulima wa nchi nzima,” alisema Bw. Samkyi.

Bw. Samkyi aliongeza kuwa mpaka sasa TADB imefanikiwa kukopesha jumla ya wakulima 1720 kutoka mikoa mitatu (3) ya wilaya saba (7) za mikoa ya mwanzo ya majaribio ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga, Iringa na Njombe.

Aliongeza kuwa TADB imejipanga kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

“Tumedhamiria na kujizatiti na kuhakikisha tunachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia wakulima wadogo na wakulima wakubwa wanaosaidia wakulima wadogo kwa kuwapatia mikopo yenye gharama nafuu,” aliongeza.

Mkurugenzi Mwendeshaji huyo alisema Benki imejidhatiti katika kufanya tathmini ya kina katika mnyororo mzima wa thamani ili kutambua mapengo na mapungufu yanayohitaji utatuzi kwa minajili ya kuongeza thamani na ushindani kwenye masoko nchi nzima.

“Sera ya TADB ni kutathmini mnyororo mzima wa thamani ili kutambua mapengo na mapungufu yanayohitaji utatuzi, na ambayo utatuzi wake utaongeza tija na uwezo wa ushindani kwenye masoko, na hivyo kukuza uchumi wa walio wengi na kupunguza umaskini nchini kote,” aliongeza.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ilizinduliwa Rasmi na Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakulima nchini, mnamo tarehe 8 Agosti 2015 mjini Lindi. Uanzishwaji wa Benki hii ni utekelezaji wa malengo ya muda mrefu ya Serikali, katika kuitikia wito wa wananchi na wadau wengine wa maendeleo ili Tanzania iweze kupiga hatua endelevu za kimaendeleo.

NEW USA:SASHA OBAMA AFANYA KAZI KWENYE MGAHAWA

SAS
Sasha Obama, bintiye Rais wa Marekani Barack Obama, ameamua kuacha ‘starehe’ za ikulu ya White House na kuanza kufanya kazi katika mgahawa mmoja, vyombo vya habari nchini Marekani vinaripoti.
Binti huyo wa umri wa miaka 15 ameanza kufanya kazi ya kuwahudumia wateja katika mgahawa mmoja ulioko Martha’s Vineyard, Massachusetts.
Sasha, ambaye anatumia jina lake kamili, Natasha, aliandamana na maafisa sita wa ulinzi wa secret service siku yake ya kwanza kazini, gazeti la Boston Herald linaripoti.
Familia ya Obama hutembelea eneo hilo sana wakati wa likizo.
Picha zinazosambazwa zinamuonesha bintiye huyo mdogo wa Obama akiwa amevalia sare ya hoteli akifanya kazi.
Mfanyakazi mmoja katika mgahawa huo aliambia gazeti hilo la Herald: “Tulikuwa tunashangaa ni kwa nini kulikuwa na watu sita walikuwa wanamsaidia msichana huyu, lakini baadaye tukagundua alikuwa nani.”

NEW SIMIYU REGIONAL:RC SIMIYU:WANUFAIKA WA TASAF WATAKAOBAINIKA KUJIHUSISHA NA ULEVI WAONDOLEWE KWENYE MPANGO

PICHA 2(1)
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo.

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini akifafanua jambo kwa wakazi wa Kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega (hawapo pichani) kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijijini hapo, Wilayani Busega Mkoani humo.
Baadhi ya wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III katika kijiji cha Mwamgoba Wilayani Busega, wakiwasikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka na katibu tawala Jumanne Sagini (hawapo pichani), walipozungumza nao kabla ya zoezi la uhawilishaji wa fedha za ruzuku kwa ajili ya mpango huo.
Bw. Methesela Mrobi akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu na viongozi wengine wa Mkoa na Wilaya(hawapo pichani) Bwawa dogo alilochimba kwa kutumia fedha za ruzuku za Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III, ambalo analitumia kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji

Mkuu wa Wilaya ya Busega , Mhe. Tano Mwera (katikati) na Katibu Tawala Wilaya ya Busega, Bw. Sebastian Masanja (kulia) wakizungumza jambo kabla ya zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III kijiji cha Mwamgoba, Wilayani Busega  (kushoto) Katibu Tawala Mkoa wa
Simiyu, Bw. Jumanne Sagini
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu , Mhe. Anthon Mtaka akimkabidhi fedha Bw. Methesela Mrobi wakati wa zoezi la uhawilishaji fedha za ruzuku kwa wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya maskini TASAF III ,katika kijiji cha Mwamgoba, Wilaya ya Busega Mkoani humo. 
       Na Stella Kalinga (Ofisi ya Mkoa wa Simiyu)
Mkuu wa  mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka amewataka viongozi wa kata na vijiji kuwabaini wanufaika wa Mpango wa kunusuru kaya TASAF III(PSSN) wanaojihusisha na ulevi na kuwaondoa katika orodha ya wanufaika wa mpango huo.
 
Mtaka ametoa agizo hilo wakati alipozungumza na wananchi wa kijiji cha Mwamgoba wilayani Busega katika zoezi la uhawilishaji fedha za TASAF III PSSN, ambapo jumla ya shilingi 2,976,000 zimegawiwa kwa wanufaika 82 kijijini hapo.
 
Mtaka amesema lengo la mpango wa TASAF III ni kuwatoa watanzania katika hali ya umaskini kwa kuwapa ruzuku itakayowasadia kupata huduma muhimu ikiwa ni pamoja huduma za afya, kuwasaidia watoto wao waweze kwenda shule lakini baadhi ya wanufaika wamekuwa wakitumia fedha hizo kulewa badala ya kuanzisha miradi midogo midogo kama ufugaji wa kuku, mbuzi na kondoo pamoja na kilimo ili miradi hiyo iwasaidie kuwaongezea kipato.
 
“Hatuwezi kuleta fedha  tukifikiri zitawasaidia kujikwamua katika Umaskini lakini mnashinda baa na vilabuni kulewa , wengine mnaongeza wake, tukiwabaini mtaondolewa kwenye huu mpango” , alisema Mtaka.
 
Mtaka amewataka wanufaika hao kujishugulisha na kilimo na ufugaji na kuondokana na dhana ya  kuwa watakuwa wanufaika wa mpango huo siku zote, ambapo alieleza azma ya  Serikali ya awamu ya tano ya kuwatoa wananchi
katika umaskini na kuwaondolea changamoto mbalimbali kama kutoa elimu ya bila malipo na kuanzisha Mfuko wa Huduma ya Afya Watanzania wasio na uwezo waweze kupata matibabu kwa gharama nafuu  na akatoa wito kwa wanufaika hao kujiunga na Mfuko wa Huduma ya Afya ya Jamii (CHF)ambao utawasaidia wao wenyewe pamoja na wategemezi wao kupata huduma za Afya katika Vituo vya kutolea huduma za Afya.
 
Aidha, ametoa wito kwa wazazi kuwakumbusha watoto wao wajibu wa kuwatunza kwa sababu kumekuwa na baadhi ya wazee ambao wametambuliwa kuwa ni maskini, wakati wana watoto wenye nguvu na uwezo wa kuwasaidia lakini hawatimizi wajibu wao kuwatunza kwa kuwapa mahitaji muhimu.
 
Akizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo Bibi. Christina Robert ambaye ni mnufaika wa mpango wa TASAF amesema mpango huo umemsaidia kuondokana na kuishi katika nyumba ya nyasi na matope na kumuwezesha kujenga nyumba ya matofali na bati.
 
“Naishukuru TASAF maana imenisaidia sana, ruzuku niliyopewa mara ya kwanza ilinisaidia kutibiwa nilipofanyiwa upasuaji, mara ya pili nilitumia tena kwenye matibabu, mara ya tatu nilinunua kuku na bata, mara ya nne  nikanunua bati nikajenga nyumba ya vyumba viwili”, alisema Christina.
 
Pamoja na kusisitiza juu ya matumizi sahihi ya fedha za ruzuku za TASAF Mtaka amewataka wananchi wa Busega na Mkoa wa Simiyu kwa ujumla kuongeza juhudi katika kilimo cha mazao ya mikunde kwa kuwa tayari Serikali ya India imekubali kununua zaidi ya tani milioni sita ya choroko, dengu na mbaazi kutoka Tanzania,  hivyo wakati utekelezaji wa makubaliano hayo utakapoanza wananchi walime kwa wingi mazao hayo kwa kuwa kutakuwa na soko la uhakika.
 
Jumla ya kaya 4260 zilibainishwa katika vijiji 41 vya wilaya ya Busega ambapo kaya 53 ziliondolewa katika mpango wa TASAF III PSSN baada ya uhakiki na kubaini kuwa hazikukidhi vigezo.

NEW LINDI REGIONAL:MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AKUTANA NA WAJASIRIAMALI WA MKOA WA LINDI

 
12
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi kwenye ukumbi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Kagwa.

Mkuu wa mkoa wa Lindi Ndugu Godfrey Zambi akisoma taarifa ya mkoa wakati wa mkutano uliowakutanisha Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi katika ukumbi wa Kanisa Katoliki la Mtakatifu Andrea Kagwa.

Wajasiriamali wa mkoa wa Lindi waliohudhuria mkutano wao na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.
                                               …………………………………….
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewahimiza viongozi wa mkoa wa Lindi wasimamie kikamilifu zoezi la utengenezaji wa madawati ili kuhakikisha madawati yanayotengenezwa yanakuwa na ubora na yanakidhi viwango vinavyotakiwa.
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo mjini Lindi Tarehe  7-Aug-2016 katika mkutano wake na wajasiriamali wa mkoa Lindi pamoja na viongozi mbalimbali wa mkoa huo.
 Makamu wa Rais amesema msukumo mkubwa wa serikali uliopo kwa sasa unalenga kuhakikisha madawati yanayotengenezwa kote nchini yanakuwa imara  huku akipongeza  jitihada kubwa zinazofanywa na serikali ya mkoa wa Lindi ya utengenezaji wa madawati ambapo mpaka sasa mkoa huo umebakisha asilimia Moja tu ya utengenezaji wa madawati hayo ili kukamilisha zoezi hilo
.
 Kuhusu mikopo kwa wajasiriamali, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa serikali italifanyia kazi ombi la wajasiriamali wa mkoa wa Lindi ambao wameiomba serikali ifanye mazungumzo na watendaji wa taasisi za kifedha nchini ili waweze kupunguza riba kwenye mikopo wanayopata kama hatua ya kuongeza hamasa kwa wananchi wengi zaidi kukopa fedha kwa ajili ya kuimarisha shughuli ujasiriamali.
 Makamu wa Rais pia amezitaka halmashauri zote nchi kutekeleza kwa vitendo mkakati wa kutenga asilimia TANO ya makusanyo ya mapato yake na kutoa fedha hiyo kwa wanawake na vijana kwenye halmashauri hizo ili waweze kuanzisha na kuendeleza miradi yao ya kiuchumi kwenye maeneo yao.

NEW MBEYA CITY:WAZIRI MKUU AITAKA TRA KUACHA TABIA YA KUWAPANDISHIA WAFANYABIASHARA KODI KIHOLELA

mbe1
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa mkoa wa Mbeya baada ya kupokea taarifa ya mkoa Agosti 7, 2016 kwenye  Ikulu ndogo ya mbeya .  Agosti 8, 2016 atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wakulima Nanenane. (Picha na Ofisi ya Wairi Mkuu)
mbe2
………………………………………………………………………………………
*Awataka wafanyabiashara kuwaripoti watendaji wanaoongeza kiwango kikubwa cha kodi kuliko inavyostahili kulipwa
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa imeitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania kuimarisha kitengo cha tathmini ili kuweka viwango halali ambavyo havitawagandamiza wafanyabiashara na uwepo uwazi kuhusu viwango stahili vya kodi wanavyotakiwa kulipa.
Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Agosti 07, 2016) wakati alipozungumza na viongozi wa mikoa ya Mbeya, Katavi, Songwe, Rukwa, Ruvuma, Iringa na Njombe mara baada ya kuwasili mkoani Mbeya kwa ajili ya kufunga maadhimisho ya maonyesho ya nane nane kwa mikoa ya Kanda ya Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika mkoani Mbeya.
‘‘TRA waendelee kukusanya mapato vizuri ila kuna wakusanya kodi wanaotaka kuharibu mkakati wa Serikali kwa kufanya mambo ya hovyo kwa kuwaongezea viwango vikubwa vya kodi kuliko kodi stahili wanavyotakiwa kulipa na kufanya suala hili liwe kama tatizo au adhabu kwao jambo ambalo si sahihi. Naagiza watendaji wa TRA wanaofanya hivyo wasakwe na wachukuliwe hatua“, alisema.
‘‘Wafanyabiashara mnaoonewa kwa chuki binafsi na watendaji wa TRA toeni taarifa ili muweze kufanya biashara zenu kwa uhakika bila ya wasiwasi lengo ni kuwafanya muweze kulipa kodi sahihi kwa mujibu wa sheria“, alisema.
Ili kufanikisha mpango huo Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya kuwasikiliza wafanyabiashara ambao wana malalamiko ya kweli ya kutotendewa haki katika kutozwa kodi kwa sababu mchango kupitia kodi ni kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa Taifa.
Katika hatua nyingine ameitaka idara ya Uhamiaji ijikite katika kudhibiti watumishi wasiokuwa waaminifu ambao wamekuwa  wakichukua rushwa kutoka kwa wageni wanaotoka nje ya nchi na kuwaingiza nchini bila ya kuwa na vibali maalumu.
‘‘Ni lazima tuhakikishe hakuna uingiaji holela ndani ya nchi na hasa kwa  wanaoingia bila vibali maalumu kwani bila ya kudhibiti suala hilo tunaacha mianya ya kuingia watu wasiokuwa na nia njema na Taifa letu. Watu watakaobainika wameingia nchini bila ya vibali wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria,“ alisema.
Alisema kitendo cha mipaka kushindwa kudhibitiwa na kuruhusu uingiaji holela wa watu wasiokuwa na vibali chini kunasababisha Serikali kushindwa kuteleza ipasavyo mipango yake ya kuwahudumia wananchi kulingana na idadi halisi.
Mbali na kuiagiza Idara ya Uhamiaji pia Waziri Mkuu alisema wakuu wa mikoa ya mipakani wana jukumu la ziada la kuhakikisha wanadhibiti mipaka yote na kuhakikisha hakuna watu wanaoingia nchini bila ya kuwa na vibali.
Hata hivyo Waziri Mkuu amewataka wakuu wa mikoa kote nchini kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yao na kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu ili Watanzania waweze kutekeleza shughuli zao za maendeleo kama walivyojipangia.
“Natambua kuwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ndio wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama katika maeneo yenu, endeleeni kuimarisha hali ya ulinzi na usalama. Nchi hii tunahitaji  iwe tulivu na salama na ni wajibu wenu kuhakikisha kwamba lolote linalotokea mnalikabili vilivyo“, alisema.
Awali Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Makalla alipokuwa akisoma taarifa ya mkoa huo kwa Waziri Mkuu alisema mkoa huo una jumla ya viwanda 1,653 kati yake vikubwa ni tisa, vya kati 19 na vidogo 1,625  na bado wanaendelea kuzisimamia halmashauri kutenga maeneo zaidi kwa ajili ya kuongeza na kupanua viwanda.
Mhe. Makalla alisema katika eneo hilo la viwanda mkoa una kiwanda kimoja cha kusindika nyama cha Tanganyika Pachers kilichopo wilayani Mbeya ambacho hakijawahi kufanya kazi tangu kilipojengwa na kufungwa mitambo mwaka 1975.
Mkuu huyo wa mkoa alisema usimamizi wa kiwanda hicho uko chini ya Masajili wa Hazina na kwamba tayari kuna muwekezaji amepatikana kwa ajili ya kukiendesha hivyo ameiomba Serikali kuharakisha taratibu za mikataba ili kiweze kuanza kufanya kazi.