Monday, 15 August 2016

NEW OATH:Manaibu Kamishina wa Jeshi la Polisi waliokuwa nje ya nchi wala kiapo cha maadili ya Viongozi wa Umma.

KIA1
Kamishia wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akiwaapisha  Manaibu Kamishina  wa Jeshi la Polisi (DCP) Modestus Gasper Lyimo na Juma Yussuf (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Manaibu Kamishina hao awakupata fursa ya kula kiapo hicho pamoja na wenzao mnamo tarehe 16 Julai 2016.
KIA2
Mwakilishi wa Katibu Mkuu Kiongozi,Charles Mwankupili akizingumza jambo wakati wa hafla ya kula kiapo cha Maadili kwa  Manaibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP) Modestus Gasper Lyimo na Juma Yussuf Ali (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda na Mwakilishi wa IGP, Kamishina wa Jeshi la Polisi Nsato Marijani Mssazya.
KIA3
Manaibu Kamishina Modestus Gasper Lyimo (kushoto) na Juma Yussuf wa Jeshi la Polisi wakila kiapo cha maadili ya viongozi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Manaibu Kamishina hao awakupata fursa ya kula kiapo hicho pamoja na wenzao mnamo tarehe 16 Julai 2016.
KIA4
Manaibu Kamishina Modestus Gasper Lyimo (kushoto) na Juma Yussuf wa Jeshi la Polisi wakitia saini katika fomu za kiapo cha maadili ya viongozi wa umma leo Jijini Dar es Salaam. Manaibu Kamishina hao awakupata fursa ya kula kiapo hicho pamoja na wenzao mnamo tarehe 16 Julai 2016.
KIA5
Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akimkabidhi fomu ya maadili ya viongozi wa umma Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP) Modestus Gasper Lyimo
KIA6
Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda akimkabidhi fomu ya maadili ya viongozi wa umma Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP) Juma Yussuf
MAD
Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda(waliokaa katikati) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi Manaibu Kamishina wa Jeshi la Polisi DCP Modestus Gasper Lyimo na DCP Juma Yussuf Ali walioapishwa leo Jijini Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Sekretaieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma.
Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO

Monday, 8 August 2016

NEW COVER PAGE IN TANZANIA MAGAZINE


20160808_051311

20160808_051317

20160808_051333

20160808_051341

20160808_051350

20160808_051358

20160808_051406

20160808_051412

20160808_051422

20160808_051428

20160808_051436

20160808_051442

20160808_051453

20160808_051459

20160808_051508

20160808_051514

20160808_051523

20160808_051529

20160808_051540

20160808_051546

20160808_051607

20160808_051614
20160808_051648

NEW FASHION:ASYA IDAROUS KHAMINI AFANYA KWELI DALLAS, TEXAS NCHINI MAREKANI

Mamaa wa mitindo Asya Idarous Khamsini akipata picha ya kumbukumbu baada ya siku ya Jumamosi Aug 6, 2016 kufanya kweli kwenye kenya Women Reunion iliyoyanyika katika hotel ya Hilton Garden Inn  iliyopo mtaa wa State Highway Dallas, Texas nchini Marekani.
Mlimbwende wa mitindo akiwa kwenye kivazi kilichowavutia wengi kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini alipofanya kweli siku ya Jumamosi Aug 6, 2016  kwenye kenya Women Reunion iliyoyanyika katika hotel ya  Hilton Garden Inn  iliyopo mtaa wa State Highway Dallas, Texas nchini Marekani.
Mlimbwende akiwa katika pozi na kivazi cha mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
Ni Kivazi kingine kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
Mlimbwende katika picha.
Mlibwende katika picha akiwa na kivazi kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
Asya Idarous Khamsini ni Balaa tupu.
Mlimbwende akiwa ametokelezea kweli na kivazi kutoka kwa mama mitindo Asya Idarous Khamsini.
Picha ya pamoja.

NEW AGRICULTURE BANK:Benki ya Kilimo yapanga kutoa huduma nchi nzima

Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi (Kulia) akizungumza na wanahabari wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kushoto) akizungumza na wanahabari wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi. Kulia ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Wapili Kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ndg. Godfrey Weston Zambi (Wapili Kulia) wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi. Wengine pichani ni viongozi waandamizi wa TADB wakiongozwa na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kushoto).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dkt. Florens Turuka (Wapili Kulia), akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Wapili Kushoto). Wengine pichani ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kushoto) na Bw. Adam Kamanda (Kulia).
Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Mhe. Nape Nnauye (Kushoto) akipata maelezo kuhusu Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kutoka kwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Kulia).
Afisa wa TADB, Bw. Victor Mziray (Kulia) akiwahudumia wateja waliojitokeza kutembelea Banda la Benki ya Kilimo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) akimsikiliza Bibi Constancia Mahanga (Kushoto) wa Kikundi Umoja kutoka Tandahimba wanaodhaminiwa na TADB.
Afisa Masoko wa Wakala wa Mbegu, Bi. Jacqueline Itatiro (Kushoto) akimuelezea namna ya Wakala huo unavyofanya kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia). Wengine pichani ni Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Wapili Kulia) na viongozi wengine wa Benki hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Kulia) akiangalia unga wa muhogo unaozalishwa na Kikundi cha Vijana cha Agripreneur. Kushoto wanakikundi wa kikundi hicho, Bw. Fortunata Mwananjela na Bi. Veronica Kichanta.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TADB, Bibi Rosebud Kurwijila (Katikati) na Mkurugenzi Mwendeshaji wa Benki hiyo Bw. Thomas Samkyi (Wapili kulia) wakimsikiliza Katibu wa Chama cha Wakulima cha Nzihi, Bw. Emmanuel Fungo anayewakilisha vikundi nane (8) vya mkoa wa Iringa waliopatiwa mkopo na TADB.


Katika kuadhimisha mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imepanga kuanza kutoa mikopo kwa wakulima wadogo na wakulima wakubwa wanaosaidia wakulima wadogo nchi nzima ili kuharakisha mapinduzi ya kilimo nchini.

Mikakati hiyo iliwekwa bayana na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki hiyo, Bibi Rosebud Kurwijila wakati wa Maonesho ya Nane Nane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Ngongo mjini Lindi.

Bibi Kurwijila alisema kuwa TADB inalenga kutelekeza kwa vitendo Maelekezo ya Serikali ya kupunguza changamoto zinazowakabili wakulima nchi kote, hivyo TADB imejipanga kuwafikia wakulima wadogo nchi nzima ili kuharakisha mapinduzi ya kilimo nchini.

“Benki imejipanga kutoa mikopo yenye riba nafuu katika muda mfupi, wa kati na mrefu kwa Wakulima wadogo wadogo, wa kati na wakubwa, hususan kuziba pengo la upatikanaji wa fedha za kwenye mnyororo wa ongezeko la thamani ili kuharakisha mapinduzi ya kilimo katika tasnia za kilimo, mifugo, uvuvi na mazao ya misitu (ufugaji nyuki),” alisema Bibi Kurwijila.

Aliongeza kuwa kwa sasa Benki imeanza kupokea maombi kutoka kwa wakulima wanaohitaji mikopo nchi nzima ili kuwakwamua na changamoto ya ufinyu mkubwa wa upatikanaji wa fedha mikopo kwa ajili ya maendeleo ya kilimo nchini.

Akizungumza katika Maonesho hayo, Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB, Bw. Thomas Samkyi alisema kwamba Benki yake imetimiza mwaka mmoja kwa kutengeneza faida kwa kupata jumla ya kiasi cha Shilingi 450 milioni kwa mwaka jana na Shilingi 1.72 bilioni kwa miezi sita (6) ya mwaka 2016.

“Benki imeanza kazi kwa kishindo kwa kutengeneza faida jambo linaloonyesha uimara wa Benki katika kuwahudumia wakulima wa nchi nzima,” alisema Bw. Samkyi.

Bw. Samkyi aliongeza kuwa mpaka sasa TADB imefanikiwa kukopesha jumla ya wakulima 1720 kutoka mikoa mitatu (3) ya wilaya saba (7) za mikoa ya mwanzo ya majaribio ambayo ni Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Tanga, Iringa na Njombe.

Aliongeza kuwa TADB imejipanga kuwa benki ya mfano na ya kisasa katika kuleta mapinduzi ya kilimo Tanzania kutoka kilimo cha kujikimu kwenda katika kilimo cha kibiashara na uzalishaji wenye tija katika kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

“Tumedhamiria na kujizatiti na kuhakikisha tunachangia kwa kiasi kikubwa katika kuleta Mapinduzi yenye tija katika Sekta ya Kilimo nchini kwa kusaidia wakulima wadogo na wakulima wakubwa wanaosaidia wakulima wadogo kwa kuwapatia mikopo yenye gharama nafuu,” aliongeza.

Mkurugenzi Mwendeshaji huyo alisema Benki imejidhatiti katika kufanya tathmini ya kina katika mnyororo mzima wa thamani ili kutambua mapengo na mapungufu yanayohitaji utatuzi kwa minajili ya kuongeza thamani na ushindani kwenye masoko nchi nzima.

“Sera ya TADB ni kutathmini mnyororo mzima wa thamani ili kutambua mapengo na mapungufu yanayohitaji utatuzi, na ambayo utatuzi wake utaongeza tija na uwezo wa ushindani kwenye masoko, na hivyo kukuza uchumi wa walio wengi na kupunguza umaskini nchini kote,” aliongeza.

Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania ilizinduliwa Rasmi na Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwenye Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wakulima nchini, mnamo tarehe 8 Agosti 2015 mjini Lindi. Uanzishwaji wa Benki hii ni utekelezaji wa malengo ya muda mrefu ya Serikali, katika kuitikia wito wa wananchi na wadau wengine wa maendeleo ili Tanzania iweze kupiga hatua endelevu za kimaendeleo.