Saturday, 4 June 2016

SERIKALI:Rais Dr. Magufuli akutana na kufanya mazungumzo na kiongonzi wa chama cha kikomonisti cha China Luo Zhijun Ikulu jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kiongonzi wa chama cha kikomonisti cha China Liu Zhjuin kutoka Jimbo la Jiangsu China,Jijini Dar es salaam

u

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa China hapa nchini Lu Youqing aliyeambatana na kiongonzi huyo wa chama cha kikomunisti cha China,Ikulu jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisaliamiana na kiongonzi wa chama cha China Luo Zhijun kutoka jimbo la Jiangsun nchini China.

Rais wa Jamhuri wa Muungano ya Tanzania akisaliamiana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda,Ikulu Jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania akiagana Kiongonzi wa Chama cha Kikomunisti cha Chini mara Baada ya kumaliza Mazungumzo leo Ikulu Jijini Dar es salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa kiongonzi wa chama cha kikomunist cha China Luo Zhijun pamoja na Balozi wa China Hapa Nchni Luo Youqing mara Baada ya kumaliza mazungumzo yao.Wengine katika picha ni katibu mkuu kiongonzi Balozi Mhandisi John Kijazi pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda.

Wednesday, 1 June 2016

MICHEZO:UCHAGUZI YANGA, MWISHO WA KUCHUKUA, KUREJESHA FOMU JUNI 6

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi wa Klabu ya Young Africans imeridhishwa na mwenendo wa wanachama kwa namna wanavyochukua na kurejesha fomu.
Katika kikao chake cha kufanya tathmini kilichoketi jioni ya leo Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, Wakili Msomi Alloyce Komba kutokana na mipango yake, imesogeza mbele mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu mpaka Jumatatu Juni 6, 2016 saa 10:00 jioni. Isipokuwa Jumamosi na Jumapili ya Juni 4 na 5, 2016.
Hadi sasa wanachama tisa (9) wamechukua na kurejesha fomu. Wanachama hao ni Aaron Nyanda na Titus Osoro wanaowania nafasi ya makamu mwenyekiti kwa mujibu wa katiba ya mwaka 2010 inayotambulika serikalini hadi sasa.
Wengine ni Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar ambao wanawania nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji. Uchaguzi wa Yanga unatarajiwa kufanyika Juni 25, 2016.
Fomu zinapatikana katika ofisi za TFF zilizoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam. Vilevile utaratibu unafanyika ili fomu ziweze kupatikana katika tovuti ya shirikishowww.tff.or.tz
Fomu zinapatikana kwa gharama ya Sh 200,000 kwa nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti na Sh 100,000 kwa wagombea wa nafasi ya ujumbe wa kamati ya utendaji. Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu ni tarehe 6 Juni, 2016. 

BIASHARA:TBL GROUP YAIBUKA MSHINDI WA KWANZA WA TUZO YA MZALISHAJI BORA WA MWAKA 2015

TBL1Rais  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.John Magufuli akikabidhi tuzo  kwa mshindi  wa kwanza wa Tuzo ya Rais ya mzalishaji bora wa mwaka 2015, kwa  Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin  wakati wa hafla ya kutoa  tuzo kwa washindi iliyofanyika jijini katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam . Wengine ni Mwenyekiti wa Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Dk. Samwel Nyantahe ( wa pili kulia)  na kushoto ni Waziri wa Biashara ,Viwanda na Uwekezaji Mh.Charles Mwijage.
TBL2Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
TBL3Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group na maofisa waandamizi wa kampuni wakifuatilia matukio wakati wa hafla hiyo
TBL4Rais John Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na watendaji wa makampuni ambayo yameshinda tuzo mbalimbali katika kipindi cha mwaka huu
TBL5Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin (wa nne mstari wa mbele kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa kampuni hiyo waliohudhuria hafla ya kukabidhiwa tuzo.
…………………………………………………………………………………………………………………
Kampuni ya  TBL Group imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya Rais ya mzalishaji bora kwa kipindi cha mwaka 2015,vilevile imeibuka mshindi wa kwanza katika kundi la uzalishaji wa vinywaji ambapo  imetunukiwa tuzo kwa ushindi huo.
Tuzo ya mzalishaji bora hutolewa na Chama Cha Wenye Viwanda Tanzania (CTI na hafla ya kukabidhi tuzo kwa washindi mbalimbali imefanyika leo jijini Dar es salaam katika  hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambapo mgeni wa heshima aliyekabidhi tuzo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mheshimiwa John Magufuli.
Akiongea baada ya hafla  hiyo Mkurugenzi Mkuu wa TBL Group,Roberto Jarrin,alisema ushindi huu ni zawadi kwa wafanyakazi wote wa kampuni  kwa kuwa jitihada za kila mmoja ndizo zimepelekea mafanikio haya kupatikana.
“Kwetu TBL Grop tunayo furaha kwa kushinda tuzo hizi tulizofanikiwa kuzinyakua siku ya leo,haya kwetu ni mafanikio makubwa na tumefurahi kuona mchango wa uwekezaji wetu unatambuliwa na tunaendelea kuwa washindi wa tuzo mbalimbali zinazotolewa na taasisi mbalimbali”.Alisema Jarrin.
Alisema TBL Group itaendelea kufanya uwekezaji zaidi nchini na kuchangia kukua kwa uchumi wa taifa ikiwemo kuunga mkono jitihada za serikali za kupunguza tatizo la ajira nchini ambapo mbali na kutoa ajira kwenye viwanda vyake na mtandao wa wafanyabiashara inaoshirikiana nao tayari imeanzisha miradi ya kuwasaidia wakulima ambayo tayari imeanza kuonyesha mafanikio kwa kubadilisha maisha ya wakulima kuwa bora.
“Tunaishukuru serikali ya Tanzania kwa kufanya kazi kwa karibu na wawekezaji na nina imani tutaendelea kushirikiana ili kuweza kupata mafanikio zaidi katika siku za usoni”.Alisema.

USAFIRI:FASTJET YATANGAZA SHINDANO LINGINE KWA WATEJA WAKE

fastjet, shirika la ndege la bei nafuu Afrika  limezifanya ndoto za usafiri  kuwa za kweli  kwa abiria wake zaidi ya milioni mbili  waliopaa anga za Afrika tangu kuzinduliwa kwake Novemba 2012.
 Ukiwa kama mkakati wa kuhamasisha hata Watanzania wengi zaidi  kusafiri, fastjet  imetangaza kwamba abiria yeyote anayenunua tiketi  kuanzia Jumanne Mei 31 ataingia kwenye  bahati na nasibu  ya kwanza ya aina yake  ijumulikanayo Big 10 draw ambapo washindi 10 watasafiri bure   katika njia yoyote  ya fastjet katika mtandao wake barani Afrika.
Kwa watu kumi watakaoshinda bahati nasibu hiyo  shirika linawapa uwezo wa kwenda katika mapumziko  au kwenda katika safari ya manunuzi  pamoja na marafiki  na familia  jambo wamekuwa wakiliwazia  kila mara.
Ama kwa wajasiriamali wa Tanzania, safari hiyo inaweza kutumia kukuza mahitaji ya biashara kwa kuokoa  gharama za usafiri katika safari nyingine kumi wanazozihitaji  kusafiri.
 “Ni rahisi, lengo la fastjet ni kufanya uwezekano kwa wateja wengi kusafiri, iwe ni kwa shughuli za biashara, kutembelea marafiki  na familia, au kufurahia burudani ya kusafiri,” alisema Meneja Mkuu wa fastjet Tanzania John Corse.
 Njia ambazo zinahusiana  kwa ajili hiyo ni safari za kutoka Dare es Salaam kwenda Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Zanzibar, Nairobi, Entebbe, Lusaka, Harare na Johannesburg hali kadhalika safari  kati ya Kilimanjaro na Harare.
 Tiketi zitakazonunuliwa Jumanne Mei 31, 20016 kwa njia za kimataifa na  za ndani  zitawawezesha abiria wake kuingia katika bahati nasibu ya Big 10. Washindi watatangazwa Juni 2016 na safari 10 za bure  ni lazima zifanyike  kabla ya Desemba 11, 2016.
 Ikitambuliwa kama shirika la ndege la gharama nafuu Afrika, fastjet hivi sasa inafanya safari  ndani ya nchi 11 kwa wafanyabiashara, watali na familia ambazo zimeipokea tozo lake la nauli nafuu na linalofikia kwa usafiri wa anga.
 “Usafiri wa anga ni ufunguo unaoendelea kuhamasisha na kukuza uchumi wa Tanzania  kwa kuufanya uwe rahisi kwa familia, wafanya biashara  na watalii kumudu kusafiri,” alisema Corse  na kuongeza, “tumezindua punguzo hili la nauli  hivyo kwamba hata wasafiri wanaweza kuzoea usafiri wa anga wanaoumudu, iwe wanasafiri kwa ajili ya biashara au mapumziko.”
Kukata tiketi kiunaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia www.fastjet.com, kupitia wakala aliyethibitishwa au kwa kuwasiliana na na fastjet kupitia +255 784 108 900. Malipo pia yanaweza kufanyika kwa fedha taslimu, kwa njia ya mtandao kwa kutumia kadi au  malipo kwa njia ya mitandao ya simu.

MICHEZO:SERIKALI KUSHIRIKIANA NA KAMPUNI YA TING KUBORESHA MAPATO YA UWANJA WA TAIFA.

tin1Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge akizungumza na wawakilishi kutoka Kampuni ya TING(hawapo pichani) kuhusu kushirikiana na Serikali kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
tin2Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos akifafnua jambo katika kikao kati ya kampuni yake na Serikali kilicholenga kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
tin3Mkuu wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah akionesha jinsi kampuni yake itakavyoweka miundombinu ya kuweka matangazo ndani ya uwanja wa taifa katika kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
tin4Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo wakifatilia kikao baina ya Serikali na kampuni ya TING kushirikiana katika kuboresha mapato ya Uwanja wa taifa kupitia matangazo.
…………………………………………………………………………………………………………….
(Picha na Raymond Mushumbusi WHUSM)
Serikali imeanza majadiliano na kampuni ya TING katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo uwanjani hapo.
Akizungumza hapo jana wakati wa kikao kati ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo na kampuni hiyo, Kaimu Mkurugenzi  Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Alex Nkenyenge amesema kuwa Serikali imefarijika kupata maombi hayo kutoka kampuni ya TING ya kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa kupitia matangazo ambayo yatawekwa katika maeneo ya uwanja huo.
“Ndugu zetu TING wamekuja na wazo zuri sana na tumelipokea na tunaahidi kuliangalia kwa jicho la tatu kwani ni fursa ya pekee kwetu, sio kuboresha mapato tu bali kutangaza uwanja wetu na kuendeleza michezo kwa ujumla” alisema Bw. Nkenyenge.
Aliongeza kuwa ni wakati sasa wa Serikali pamoja na Wananchi kufaidika na uwanja wao ambao ni wa kipekee katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kwani fursa hiyo itasaidia pia kuendeleza Kijiji cha Michezo Changamani ambao pia ni mpango wa Serikali katika kuendeleza sekta ya michezo nchini.
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu kutoka TING Mch. Dkt. Veron Fernandos amesema kuwa kampuni yake itatoa ushirikiano kwa Serikali kupitia Wizara na ni azma yao kuona wananchi wanaona faida ya kuwa na uwanja wa kisasa ambao utawaletea mafanikio katika maendeleo ya michezo nchini.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani wa Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Esther Yonael ameipongeza kampuni ya TING kwa kuona fursa na kuitumia kwani kuna kampuni nyingi zinaweza kuwa ziliona hiyo fursa hii lakini sikakosa uthubutu wa kuleta maombi Wizarani kushirikiana katika suala hilo ambalo linafaida kwa pande zote mbili.
Aidha, Mkuu wa Masoko kutoka TING Bi. Bernice Hannah ameihakikishia Serikali kuwa wamejipanga vizuri na wamefanya utafiti wa kina wa mradi huo na kuona kuwa unawezeka ukafanyika na kuleta mabadiliko katika sekta ya michezo nchini.
Kampuni ya TING imedhamiria kushirikiana na Serikali katika kuboresha mapato ya uwanja wa Taifa na imejipanga kuwekeza Shilingi Billioni moja kwa miaka minne katika miundombinu na wataalam.

SERIKALI:MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AHUTUBIA MKUTANO WA UMOJA WA MATAIFA WA KUWEZESHA WANAWAKE KIUCHUMI NCHINI PAPUA NEW GUINEI LEO

un1Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mzungumzaji Mkuu wa Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye mkutano huo uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea.
un2Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipongezwa na  Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo wakati Makamu wa Rais alipomaliza kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano huo. Katikati Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Mhe. Natumbo Nandi Ndaitwah.
un3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo wakati Makamu wa Rais alipomaliza kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye Mkutano huo. Katikati Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Mhe. Natumbo Nandi Ndaitwah.
un4Rais Mstaafu wa Nigeria General Olibegan Obasanjo akimpongeza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan baada ya  kuhutubia Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi kwenye mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo.
un5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Mzungumzaji Mkuu wa Mkutano wa kuwezesha Wanawake Kiuchumi katika mkutano wa nane kwa Wakuu wa Nchi za Afrika, Caribean na pacific ACP Mhe. Samia Suluhu Hassan, akihutubia kwenye mkutano huo uliofanyika leo Juni 01,2016 katika kituo cha mikutano cha kimataifa PCC Nchini Papua New Guinea. Makamu wa Rais amemuwakilisha Rais Dkt. John Magufuli kwenye mkutano huo