Thursday, 28 July 2016
NEW FAREWELL:BALOZI WA CANADA NCHINI AAGANA NA WAZIRI WA NISHATI NA MADINI PROFESA SOSPETER MUHONGO
BIG BROTHER IN A STATE:MAJALIWA AZUNGUMZA NA WATUMISHI TEMEKE
NEW AFRICA:“TUNAWEZA KUBADILISHA MAISHA YA WAAFRIKA KAMA TUKIACHA BIASHARA ZA MAGENDO”- THABO MBEKI
Raisi wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki amezungumzia biashara ya magendo ya madini ya Tanzanite katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) kuzungumzia namna ya kuzifanya biashara kuleta mabadiliko chanya barani Afrika.
Mbeki ameyasema hayo katika kongamano hilo lililowakutanisha viongozi mbalimbali wa Afrika kujadili jinsi biashara inavyoweza kusaidia kubadili maisha ya Waafrika lililofanyika leo katika hoteli ya Hyatt Regency-Kilimanjaro, Dar es salaam.
Aidha, Mbeki amesema takribani dola milioni 800 hupatikana kila mwaka kwa kuuza na kusafirisha madini ya Tanzanite nchi za nje, lakini kutokana na biashara za magendo na wizi wa madini ya Tanzanite ni dola milioni mia tano tu hupatikana kila mwaka nchini Tanzania
Ameongeza kuwa Tanzania inasafirisha kiwango kidogo cha madini hayo ukilinganisha na uchimbaji halisi unaoendelea kila mwaka, na hivyo kufanya sekta ya madini pamoja na biashara kuzorota kwa hali ya juu
Tanzania ni nchi pekee duniani inayochimba madini ya Tanzanite yenye thamani kubwa lakini nchi za Afrika Kusini na Kenya ndiyo zimekuwa zikijulikana kwa uuzaji wa madini hayo.
Mkutano huo unataraji kufanyika kwa siku mbili na kudhaminiwa na mashirikia na taasisi mbalimbali ikiwepo Taasisi ya Mo Dewji (Modewji Foundation.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Mh. Benjamin William Mkapa akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki (hawapo pichani) wa Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Rais wa Jumuiya ya wafanyabiashara wa Madini nchini Afrika Kusini, Sipho Nkosi akitoa hotuba kwenye Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Rais mstaafu wa Afrika Kusini Mh. Thabo Mbeki akichangia mada katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Kutoka kushoto ni Rais wa zamani wa Namibia, Mh. Hifikepunye Pohamba, Rais wa zamani wa Mozambique, Joaquim Chissano, Rais mstaafu, Mh. Benjamin William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mh. Thabo Mbeki pamoja na Rais wa zamani wa Mozambique, Mh. Armando Guebuza wakiwa meza kuu katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Mwakilishi wa Vijana kutoka nchini Nigeria akishiriki kwenye Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lililoanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Mfanyabiashara na mmliki wa makampuni ya Excel Management, Mikono Speakers na Focus Outdoor Deogratius Kilawe akitoa maoni katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) ulioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Mawaziri wakuu wastaafu kutoka kushoto ni Mh. Salim Ahmed Salim, Mh. John Malecela pamoja na Mh. Cleopa Msuya walikuwa miongoni mwa wageni waalikwa katika Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) ulioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro.
Pichani juu na chini ni wadau mbalimbali walioshiriki kwenye Kongamano la Viongozi wastaafu wa Afrika 2016 (African Leadership Forum 2016) lilioanza leo jijini Dar Es Salaam katika Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro na kuratibiwa na Uongozi Institute.
Wednesday, 27 July 2016
BUGURUNI SCENE:MBUNGE WA SEGEREA BONNAH KALUWA AREJESHA KIWANJA KWA WANANCHI WA KATA YA BUGURUNI
Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kaluwa (kulia), akizungumza Dar es Salaam leo na wafanyakazi wa Kampuni ya M/S Yassa General Supplies Limited iliyokodishwa kiwanja kilichopo nyuma ya Kituo cha Polisi Buguruni ambapo ametoa siku tatu waondoke kupisha ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Buguruni. Mapato ya kiwanja hicho kwa zaidi ya miaka 10 yalikuwa hayajulikani yalipokuwa yakienda.
Ofisa Mtendaji wa Kata ya Buguruni, Remmy Mishehe (kulia), akitoa ufafanuzi kwa wanahabari kuhusu kiwanja hicho.
Maelezo zaidi yakitolewa.
Mmoja wa mtu aliyedaiwa ni dereva wa kampuni hiyo, akidhibitiwa baada ya kudaiwa kutoa lugha ambayo siyo nzuri mbele ya mbunge wakati wa ziara ya mbunge huyo kukagua kiwanja hicho.
Malori ya kampuni hiyo yakiwa yameegeshwa kwenye kiwanja hicho.
Mmoja wa viongozi wa kampuni hiyo akitoa maelezo kwa Mbunge Bonnah Kaluwa (kushoto). Katikati mwenye suti ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Kata ya Buguruni, Barua Mwakilanga.
…………………………………………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonnah Kaluwa amefanikiwa kukirejesha kiwanja kwa wananchi wa Kata ya Buguruni kilichokuwa kikitumika kuegesha magari kwa malipo bila kujulikana matumizi ya fedha hizo.
Kiwanja hicho ambacho kipo nyuma ya kituo cha Polisi Buguruni kilikuwa kimetengwa miaka mingi iliyopita kwa ajili ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Buguruni.
Akizungumza wakati akikagua kiwanja hicho Dar es Salaam leo asubuhi ambacho kinatumiwa na Kampuni ya M/S Yassa General Supplies Limited kuegesha magari yao alisema wametoa siku tatu wawe wameondoka ili waanze mara moja ujenzi wa shule hiyo ambapo jumla ya sh. milioni 40 za kuanzia ujenzi huo zimetengwa.
“Kata ya Buguruni haina shule hata moja ya sekondari kupatikana kwa kiwanja hiki kitasaidia watoto kupata shule katika kata yao badala ya kwenda shule zingine za mbali” alisema Kaluwa.
Kaluwa aliongeza kuwa waliokuwa wakitumia kiwanja hicho waliingia mkataba na uongozi wa Kata ya Buguruni ambapo katika kipengere namba nne kilieleza kuwa ikifika wakati eneo hilo likihitajika basi mpangaji atalazimika kuondoka.
“Kwa kuwa mpangaji wa eneo hilo yupo na mkataba unajieleza wenyewe kupitia kipengere hicho tunaomba wahusika watupishe haraka iwezekanavyo tuanze ujenzi wa sekondari” alisema Kaluwa.
ELDERLY: SERIKALI YAZITAKA FAMILIA ZENYE UWEZO KUTOKWEPA JUKUMU LA KULEA WAZEE NA WATU WENYE ULEMAVU.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisaini kitabu cha wageni alipotembelea kambi ya kulea wazee ya SukaMahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida, Kulia ni Bw. Richard Mallya Mkurugenzi Idara ya Ununuzi na Ugavi kutoka Wizara hiyo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akimueleza jambo Afisa Mfawidhi wa kambi ya kulea wazee ya Sukamahela Bw. Jeremiah Paul
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Wazee wanaoishi katika kambi ya kulea wazee ya Sukamahela na kuwaeleza dhumuni la serikali la kuzisaidia kambi hizo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akimkabidhi moja ya Mzee katika kambi ya wazee ya Sukamahela boksi la sabuni kwa niaba ya wazee katika kituo hicho chenye jumla ya wazee 67.
Viongozi wa Kambi ya kulea Wazee ya Sokamahela wakimuonesha Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga baadhi ya nyumba wazazoishi wazee ambapo sehemu ya nyumba hizo zipo kwenye hali mbaya za kuhitaji marekebisho.
Baadhi ya Wazee wanaoishi katika kambi ya Sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akisalimiana na Bi. Theresia Msiwa anayeishi katika kambi ya kulea wazee ya SukaMahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida
Jengo la Zahanati ya Serikali ya Sukamahela iliyo karibu na kituo hicho ambayo pia inasaidia kutoa kuhuma za matibabu kwa wazee wa kituo hicho.
Muuguzi katika Zahanati ya Sukamahela Bi.Marry Sailale akimpa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga wa shughuli mbalimbali anazofanya ikiwemo kuwahudumia Wazee wanaoishi katika kambi ya Wazee ya Sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Muuguzi katika Zahanati ya Sukamahela Bi.Marry Sailale akisalimiana na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga alipotembelea kambi ya kulea wazee ya Sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akiwaaga Wazee katika kambi ya kulea wazee ya SukaMahela baada ya kutembelea na kuona hali halisi ya Mazingira katika kambi hiyo.

Baadhi ya nyumba zilizo katika kambi ya kulea wazee ya sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba Nkinga akimpa maelekezo Afisa Mfawidhi wa kambi ya kulea wazee ya Sukamahela iliyopo Wilayani Manyoni Mkoani Singida Bw. Jeremiah Paul (kushoto)na kumtaka kuwa makini katika kupokea Wazee katika kambi hiyo kwani kumekuwa na tabia ya Vijana wenye uwezo kupeleka wazazi wao kwenye kambi hizi na kukwepa jukumu la kuwalea,Kulia ni Bw. Richard Mallya Mkurugenzi Idara ya Ununuzi na Ugavi kutoka Wizara hiyo.
Subscribe to:
Comments (Atom)















