Monday, 1 August 2016

NEW DECISION:SERIKALI YATOA SIKU 30 KWA GGM KUTOA UAMUZI

ggm1Afisa Madini wa Geita, Fabian Mshai (aliyesimama) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati), namna ambavyo Ofisi yake ilitekeleza maagizo aliyoyatoa kwao kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) likiwemo suala la mipasuko ya nyumba zao. Wengine pichani ni maafisa kutoka Wizarani.
ggm2Baadhi ya Maafisa kutoka Wizara ya Nishati na Madini wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (hayupo pichani), wakati alipokuwa akizungumza na uongozi wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi kuhusu ripoti ya wataalam wa mipasuko kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) juu ya chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba na majengo yaliyo karibu na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM).
ggm3Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani akizungumza na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani kuhusu uamuzi wa Serikali kufuatia malalamiko mbalimbali yaliyotolewa na baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwa shughuli zinazoendeshwa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna mbalimbali.
ggm4Mbunge wa Viti Maalum Geita (CHADEMA), Upendo Peneza, akizungumza wakati wa kikao baina ya Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani husika kuhusu malalamiko mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwamba shughuli zinazofanywa na Mgodi huo zinawaathiri kwa namna mbalimbali.
ggm5Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani (katikati) akitoa maagizo mbalimbali kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuhusu malalamiko ya baadhi ya wananchi wanaoishi jirani na Mgodi huo kuwa shughuli zinazofanywa na Mgodi zinawaathiri kwa namna mbalimbali. Waliokaa Kulia ni viongozi kutoka GGM. Kushoto ni baadhi ya wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani na Maafisa wa Wizara ya Nishati na Madini.
…………………………………………………………………………………………………..
Na Veronica Simba – GEITA
Serikali imetoa siku 30 kwa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kuwalipa fidia wananchi wanaoishi ndani ya eneo la leseni ya Mgodi huo au kuwaruhusu rasmi waendelee kuishi humo na kufanya shughuli za kiuchumi.
Sambamba na agizo hilo, pia Serikali imeupa Mgodi huo siku 14 kuziba Tuta lililopasuka ambalo huzuia maji machafu kutoka Mgodini yasiende katika makazi ya wananchi.  
Aidha, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na timu ya wataalam wa mitetemo kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), baada ya kukamilisha kazi waliyopewa kutafiti chanzo cha mipasuko ya baadhi ya nyumba za wananchi na majengo mbalimbali yaliyo jirani na Mgodi wa GGM, Serikali imeagiza timu hiyo kufanya tathmini maalum ya idadi ya waathirika.
Iliagizwa kazi hiyo ifanyike kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Kitengo cha Maafa na Kitengo cha Mazingira pamoja na uongozi kuanzia ngazi za vijiji mpaka madiwani na wabunge husika kwa muda wa siku Saba tu kuanzia tarehe 29 mwezi huu na kuiwasilisha serikalini ili hatua stahiki zichukuliwe.
Maagizo hayo yalitolewa hivi karibuni mjini Geita na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt Medard Kalemani katika kikao chake kilichomshirikisha Mkuu wa Mkoa wa Geita na wawakilishi wa wananchi wa Geita wakiwamo wabunge na madiwani.
Dkt Kalemani alisema kuwa maagizo hayo ni kufuatia maelekezo aliyoyatoa mapema mwezi Februari mwaka huu alipotembelea mkoani humo na kusikiliza kero za wananchi wa vitongoji vya Katoma na Nyamalembo. Alisema maagizo hayo yasipotekelezwa ipasavyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa, chini ya sheria ya madini na sheria nyingine za nchi.
Akifafanua zaidi kuhusu masuala hayo yaliyosababisha Serikali kufikia hatua husika, Naibu Waziri alisema kuwa mwezi Februari alipotembelea Geita, wananchi walieleza kero kubwa walizokuwa nazo kuwa ni baadhi ya nyumba zao kupasuka kiasi cha kutoweza kukalika na nyingine kukalika lakini zimeharibika kutokana na ulipuaji wa baruti (blasting) wa Mgodi wa GGM.
Malalamiko mengine yalihusu wananchi ambao wanaendelea kuwa na makazi ndani ya eneo la leseni ya GGM, ambayo ina ukubwa wa kilomita za mraba 196. 7 ambao walikuwa wanadai fidia ili waondoke katika eneo husika au waendelee kubaki na kufanya shughuli zao za maendeleo.
Pia, baadhi ya wananchi wanaoishi karibu na Mgodi na hasa maeneo ya chini ya Mgodi, walilalamikia maji machafu ambayo yalikuwa yanakingwa na tuta ambalo lilikuwa limebomoka na kuruhusu maji kutiririka kuelekea kwenye makazi yao na hivyo kuwepo uwezekano wa kuathiri afya zao. Walitaka hatua madhubuti zichukuliwe kuzuia mtiririko huo wa maji.
Alisema kuwa, baada ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili, kwa suala la mipasuko, aliunda timu ya wataalam wa Serikali kutoka GST na kuiagiza kufanya utafiti wa kisayansi ili kubaini chanzo cha mipasuko husika kwa kushirikiana na wawakilishi wa wananchi wa maeneo hayo.
Timu hiyo ilikamilisha kazi hiyo na kukabidhi taarifa yake kwa Serikali mwezi Julai mwaka huu ambapo ilibainisha vyanzo vikuu viwili vya mipasuko hiyo kuwa ni udhaifu wa majengo yaliyoathirika lakini pia milipuko inayofanywa na GGM hasa ya miaka ya nyuma hususan kuanzia mwaka 2007 hadi 2010 ambayo ilikuwa na kipimo cha juu cha mitetemo kinachofikia 57.
Kuhusu wananchi wanaoishi kwenye eneo la leseni, Dkt Kalemani alisema kuwa alimwagiza Afisa Madini wa Geita kuwaandikia GGM ili wathibitishe kwa maandishi kati ya kuwaondoa wananchi wale kwa kuwafidia kama eneo hilo lilivyo kwenye leseni yao au kuwaruhusu waendelee kuishi na kufanya shughuli za maendeleo, jambo ambalo Mgodi haukutekeleza badala yake walisema wananchi hao ni wavamizi.
Aidha, kuhusu suala la Tuta, Naibu Waziri alieleza kuwa, aliagiza lizibwe mara moja ili kuepusha madhara ambayo yangeweza kujitokeza kama maji yangeendelea kutiririka kuelekea kwenye makazi ya wananchi, ambalo pia halijatekelezwa hadi sasa.
“Ni kutokana na hali hiyo, sasa Serikali tumeona tutoe maagizo ya mwisho ili yatekelezwe na yasipotekelezwa, hatua kali za kisheria zitachukuliwa.”
Naibu Waziri alisema kuwa Serikali haina nia mbaya kwa Mgodi husika isipokuwa ni wajibu wa Serikali kuhakikisha pia sheria zinafuatwa ili pande zote zipate haki stahiki.
“Tunapenda sana wawekezaji muwekeze kwa sababu ndiyo mnatupa ajira, mnalipa mirabaha na kodi lakini lazima tuzingatie sheria.”
Dkt Kalemani alizitaka Mamlaka zinazohusika kusimamia zoezi hilo kikamilifu.

NEW MAP:KATIBU MKUU WIZARA YA UJENZI NA BALOZI WA ITALIA WAKIKAGUA RAMANI YA BARABARA

BEN1Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga kushoto  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia.
BEN2Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
BEN3Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama
BEN4Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia masuala ya Ujenzi Injinia Joseph Nyamhanga  akimuonyesha Balozi wa Italia Bwana Roberto Mengoni( kulia) baadhi ya barabara ambazo zimependekezwa kuombewa mkopo wa masharti nafuu kutoka serikali ya Italia, kushoto ni Mkurugenzi wa barabara nchini Injinia Ven Ndiyamukama

PRESEDAR VISIT:RAIS DKT MAGUFULI AHITIMISHA ZIARA YA SIKU NNE MIKOA YA SINGIDA, TABORA NA SHINYANGA

GEI1Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
GEI2Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Mbunge wa Chato na Naibu Waziri wa Nishati na Mdini Mhe. Dkt Medard Kalemani baada ya kuhutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
GEI3Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika picha ya pamoja na madiwani na viongozi wa Katoro na Buseresere baada ya kuhutubia wananchi wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
GEI4Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akimsabahi mtoto Shabani Kalemani (miezi 8) na mama yake Asha  Simon baada ya kuhutubia wananchi wa Katoro na Buseresere wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
GEI5Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akilakiwa kwa furaha kijijini Bwanga  wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016
GEI6Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akisalimia wananchi  kijijini Bwanga  wakati akielekea nyumbani kwake Chato mkoani Geita leo Agosti 1, 2016

NEW PAROLE LEADER:MREMA AKUTANA NA MADEREVA BODABODA WA KINONDONI.

MRE1Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati)akisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenekiti wa Waendesha Bodaboda na Bajaj wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede na kushoto ni Katibu wake Bw. George Mbwale.
MRE2Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema ( Mwenye Kofia Katikati) akisisitiza jambo kwa madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
MRE3Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema wakati akizungumza na  madereva wa pikipiki toka Wilaya ya kinondoni wakati alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam
MRE4Mwenyekiti wa Madereva wa pikpiki Wilaya ya Kinondoni Bw. Almano Mdede akifafanua jambo kwa madereva pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (katikati) alipowatembelea madereva hao na kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam,kushoto ni Katibu wa Madereva Pikipiki Wilaya hiyo Bw. George Mbwale.
MRE5Baadhi ya madereva Pikipiki wa Wilaya ya Kinondoni wakimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Parole Mhe. Augustine Mrema (hayupo pichani) alipokutana nao ili kusikiliza kero mbalimbali wanazokutana nazo wakiwa katika kazi zao mapema hii leo jijini Dar es Salaam. 

NEW SEASON OF 8 8:MAJALIWA AFUNGUA MAONYESHO YA NANENANE MOROROGORO

NAN1Waziri Mkuu,  Kassim Majaliwa akisikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva wakati alipotembelea Banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika Monyesho ya Wakulima Nane  mjini Morogoro Agosti 1, 2016,    Kushoto ni mkewe Mary. ( Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN2Waziri Mkuu, Kassim Majliwa na Mkewe Mary (kulia kwake)wakitazama kilimo cha mbogamboga kwa mtindo wa kilimo kichuguu  wakati walipotembelea banda la Chuo Kikuucha Kilimo cha Sokoine (SUA) kwenye maonyeshoya Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN3Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama viatu vilivyotengenezwa katika gereza la Karanga  mkoani Kilimanjaro wakati alipotembelea  banda la Magereza katika  maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoroo Agosti 1, 2016, kulia ni  Mratibu wa Magereza wa maonyesho hayo na Mkuu wa Gereza la  Mtego wa Simba, Oman Msekwa. (Picha  na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN4Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na mkewe Mary (Kulia kwake) wakatazama bwawa la samaki  na banda la kufugia  bata  wakati alipotembelea banda la Magereza katika monyesho ya  wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. (Picha na Ofisi ya waziri Mkuu)
NAN5Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa na Mkewe Mary wakitazama mboga zilizokaushwa na mtambo wa kukaushia mboga hizo  katika  katika maonyesho ya wakulima Nanene nane  mjini Morogoro Agosti 1, 2016. (Picha na Ofisi a waziri Mkuu)
NAN6Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua Banda la Maonyesho la wilaya ya  Temeke  kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. Kushoto ni mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN7Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua Banda la Maonyesho la wilaya ya  Temeke  kwenye maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agosti 1, 2016. Kulia kwake ni mkewe Mary  na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam , Paul Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
NAN8Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama bidha mbalimbali  zinazotokana na zao la mronge zikiwema, dawa, mafuta na sabuni wakati alipoembelea meza ya Bibi Salome Kaiza   (kulia) kwenye banda la wilaya ya Tameke katika  maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro, Agosti, 1, 2016.  Kulia kwake ni Mkewe Mary. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN9Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakitazama matikiti maji wakati walipotembelea meza ya Bwana Diocresty Theonesy kwenye banda la wilaya ya Temeke katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN11Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakipokezana  tikiti maji wakiwa kwenye meza ya Bwana  Diocresty Theonesy kwenye banda la Wilaya ya Temeke katika Maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAN12 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary wakikagua mtama uliopandwa kwenye eneo la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika maonyesho ya wakulima Nanenane mjini Morogoro Agost 1, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

NEW GATE SYSTEM IN NATIONAL GROUND:NAIBU WAZIRI MH. ANASTAZIA WAMBURA AKAGUA ENEO LA UJENZI WA MAGETI YA KIELETRONIKI KATIKA UWANJA WA TAIFA LEO

WU1Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (kulia) akimuonesha Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura eneo eneo la ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Agosti 1, 2016 Jijini Dar es Salaam.
WU2Kaimu Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.Julius Mgaya (kulia) akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura na Katibu Mkuu Wizara ya hiyo Prof Elisante Ole Gabriel kuhusu ujenzi wa mageti ya kieletroniki katika Uwanja wa Taifa leo Agosti 1, 2016  Jijini Dar es Salaam.

NEW CANDIDATE IN OLYMPIC:WANAMICHEZO WAASWA KUTOTUMIA DAWA ZA KUONGEA NGUVU KATIKA MICHEZO.

 Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.
Alex Nkenyenge akizungumza katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda
kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika
mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.
 Mkurugenzi Mkuu wa Multichoice Tanzania Bw.
Maharage Chande  akishukuru Serikali kwa
fursa ya kuunga mkono jitihada za kuendeleza michezo wakati wa hafla ya kuwaaga
wanamichezo wanaokwenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016
leo Agosti 1, 2016.
 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na
Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akizungumza na wanamichezo na wadau wa
michezo  katika hafla ya kuwaaga
wanamichezo wanaoenda kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016
leo Agosti 1, 2016.
 Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
 Anastazia Wambura akiongea na wanamichezo na wadau wa michezo  katika hafla ya kuwaaga wanamichezo wanaokwenda
kuiwakilisha Tanzania nchini Brazil  katika
mashindano ya Olimpiki kwa mwaka 2016 leo Agosti 1, 2016.