Thursday, 26 May 2016

MICHEZO:YANGA WALIVYOPOKEA KOMBE LAO LA PILI KWA KUIFUNGA AZAM FC BAO 3-1 UWANJA WA TAIFA

MMG_6402 copyRais wa Shirikisho la soka nchini, Jamal Malinzi akimkabidhi Kombe la Ubingwa wa Shirikisho (ASFC), Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub, mara baada ya kutwaa ubingwa huo kwa kuichapa Timu ya Azam FC, Bao 3-1, katika mchezo uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar es salaam. 
MMG_6429 copyWachezaji wa Timu ya Yanga pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kutwaa Kombe la Shirikisho, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana

MICHEZO:Serengeti boys wamaliza nafasi ya tatu



Timu ya vijana ya Tanzania Serengeti Boys imemaliza katika nafasi ya tatu katika michuano maalumu ya vijana yaliyofanyika huko Goa nchini India.
Serengeti boys walishinda mchezo Wa mwisho dhidi ya Malaysia kwa 3-0 maboa ya vijana wa timu hiyo yalifungwa na Rashid Abdallah, , Shabani Zuberi, na Muhsini Malima,
AIFF Youth Cup ni Mashindano yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka la India, All India Football Federation mahsusi kuitayarisha Timu yao ya U-17 kwa ajili ya Mashindano ya yanayowakabili.
Michuano hii imetumika kuwapa vijana na timu ya Serengeti mazoezi kujianda na mchezo wao wa kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Africa dhidi ya Shelisheli .

Raymond - Natafuta kiki new song 2016

AFYA:Madaktari Tanzania wafanya upasuaji wa kihistoria

Upasuaji
Madaktari wamewafanyia upasuaji wagonjwa wawili

Madaktari wa Tanzania katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakishirikiana na wenzao wa India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa moyo wa aina yake Tanzania.
Upasuaji huo ujulikanao kama ‘bypass surgery’ ulishirikisha kupandikizwa kwa mishipa ya damu kutoka sehemu nyingine ya mwili moyoni bila kutumia mashine ya kusimamisha moyo na mapafu.
Kwa kawaida madaktari wanasema upasuaji wa moyo hufanyika baada ya moyo na mapafu kusimama, lakini upasuaji huo ulifanyika wakati moyo na mapafu vikifanya kazi.
Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa Bashir Nyangasa ameambia BBC kuwa upasuaji huo wa kupandikiza mishipa ya damu nje ya mshine ni wa kihistoria nchini Tanzania.
“Mgonjwa anaweza kutolewa mishipa ya damu kutoka miguuni au mikononi baada ya kupewa dawa ya usingizi na mishipa hiyo kupandikizwa kwenye mshipa wa moyo uliokuwa umeziba ili kuruhusu mzunguko wa damu wa moyo kama kawaida bila kutumia mashine,” amesema.
Upasuaji huo wa moyo kwa njia ya kupandikiza umefanyika kwa watu wawili, ambao umeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa hali zao zinaendelea vizuri .
Dkt Nyangasa amesema kwa sasa hakuna haja ya Watanzania wenye matatizo ya moyo kwenda nje ya nchi kwa kuwa wao kama wataalam wameweza kufanya upasuaji huo.
Anasema madaktari sasa wanaweza kuhudumia wagonjwa wengi zaidi wenye uhitaji na kupunguza gharama kwa serikali ya kusafirisha wagonjwa wa moyo nje ya nchi.
Mwandishi wa BBC aliyepo Dar es Salaam Esther Namuhisa anasema wengi wa wagonjwa wamekuwa wakisafiri hadi India ambapo wengi hukumbana na changamoto nyingi kupata huduma hiyo kifedha na hata kwenye upande wa lugha.

Monday, 23 May 2016

MICHEZO(HALMASHAURI YA KINONDONI):Meya wa Kinondoni ametoa ahadi ya kusimamia michezo kikamilifu na kuinua vipaji vya vijana

Manispaa ya kinondoni imeahidi kusimamia sekta ya michezo kikamilifu ili kuinua vipaji vya vijana katika manispaa ya kinondoni ,Hayo yamesemwa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob wakati wa kufungwa kwa mashindano ya Umoja wa Michezo ya sekondari Tanzania(UMISETA) kwa wilaya ya kinondoni yaliyofanyika shule ya sekondari Makongo Jumapili 22/05/2016,Ikiwa zimeshirikishwa shule kutoka majimbo matano ya Dar es salaam.Akiongea Mstahiki Meya amesema Halmashauri inapambama kurudisha maeneo ya wazi yaliyochukuliwa na matajiri ili vitumike kwa ajili ya michezo katika kukuza vipaji vya vijana katika manispaa ya kinondoni amemtaka afisa elimu sekondari wa manispaa ya Kinondoni kuangalia viwanja ambavyo vimeharibikaachukue greda la manispaa lipo ili viwanja vichimbwe na vijana waweze kucheza katika hali nzuri.


Mstahiki Meya wa halmashauri ya kinondoni Mh. Boniface Jacob akiongea wakati wa kufunga mashindandano.
"Tukiwa serious na michezo kwa kuandaa na kulinda maeneo ya wazi yaliyoyotengwa kwa ajili ya michezo vijana watapata fursa ya kucheza na kuonyesha vipaji vyao kisha kujitengenea ajira"
"kinondoni inamiliki timu ya mpira ya miguu inaitwa KMC timu ambayo ipo darja la kwanza ,mwaka huu imemaliza nafasi ya pili timu hiyo haina kocha,haina meneja,Meya nasema hii ni mojawapo ya fursa ya ajira kwa walimu waliopoa hapa wakifanikiwa kupata nafasi hiyo watakuwa wameajiriwa kuwa watumishi wa halmashauri ya kinondoni kwa kupewa mshahara na mktaba wa mwaka mmoja mmojana timu hii ni ya wananchi inaendeshwa kwa kutumia kodi za wananchi kwani timu imerudishwa kwa wananchi,na tunategemea kuanzaa ligi mwenzi wa nane na wachezaji watoke kinondondoni"alisisitiza Meya
"Manispaa inatoa motisha kwa timu,kila mchezaji akifunga goli anapewa milion 1 na huwa natoa milioni 3 kama motisha endapo timu itashinda,Timu ina Bus la kisasa ambalo hupeleka timu popote katika kushiriki katika mashindano mbalimbali,nategemea kwa siku za mbele KMC itacheza ligi kuu ya Tanzania Kwa hiyo vijana chezeni kwa Bidii mkijua kinondoni michezo inapewa kipaumbelee cha hali ya juu"Amesema Mstahiki Meya

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Kinondoni Mh.Boniface Jacob akikabidhi kikombe kwa Nahonda wa shule ya sekondari Makongo .

Saturday, 21 May 2016

MIKOANI NYANDA ZAJUU MWANZA: NAPE ATOA WITO WA WA ELIMU YA UOKOAJI IFUNDISHWE MASHULENI



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto), Flaviana Matata na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba wakiweka shada la maua kwenye kaburi la pamoja ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoaja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba wakijiandaa kuwasha mishumaa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto) akiweka mshumaa kwenye kaburi pamoja na Flaviana Matata kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa MV. Bukoba ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kulia) akimsikiliza Flaviana Matata muda mfupi kabla ya kupiga picha ya pamoja za kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
Picha ya Pamoja.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa kuangalia mazoezi ya uokoaji majini yaliyofanywa na vijana 50 waliohitimu mafunzo ya uokoaji yaliyodhaminiwa na Flaviana Matata Foundation pamoja na UTT wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba yaliyofanyika mjini Mwanza ambapo mamia ya watu walifariki akiwemo mama mzazi na binamu wa Flaviana Matata.
Sehemu ya waliofuzu mafunzo ya uokoaji wakionyesha namna ya kuokoa watu majini wakishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, Mhe. January Makamba Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula na Flaviana Matata
Sehemu ya makaburi ya pamoja ya waliofariki kwenye ajali ya MV. Bukoba mwaka 1996 ambapo leo imetimia miaka 20 tangia ajali hiyo imetokea.
Viongozi wa Dini walioshiriki kwenye kutoa ibada maalum ya kumbukumbu ya miaka 20 tangia kutokea kwa ajali ya MV. Bukoba