
Mstahiki Meya wa halmashauri ya kinondoni Mh. Boniface Jacob akiongea wakati wa kufunga mashindandano.
"Tukiwa serious na michezo kwa kuandaa na kulinda maeneo ya wazi yaliyoyotengwa kwa ajili ya michezo vijana watapata fursa ya kucheza na kuonyesha vipaji vyao kisha kujitengenea ajira"
"kinondoni inamiliki timu ya mpira ya miguu inaitwa KMC timu ambayo ipo darja la kwanza ,mwaka huu imemaliza nafasi ya pili timu hiyo haina kocha,haina meneja,Meya nasema hii ni mojawapo ya fursa ya ajira kwa walimu waliopoa hapa wakifanikiwa kupata nafasi hiyo watakuwa wameajiriwa kuwa watumishi wa halmashauri ya kinondoni kwa kupewa mshahara na mktaba wa mwaka mmoja mmojana timu hii ni ya wananchi inaendeshwa kwa kutumia kodi za wananchi kwani timu imerudishwa kwa wananchi,na tunategemea kuanzaa ligi mwenzi wa nane na wachezaji watoke kinondondoni"alisisitiza Meya
"Manispaa inatoa motisha kwa timu,kila mchezaji akifunga goli anapewa milion 1 na huwa natoa milioni 3 kama motisha endapo timu itashinda,Timu ina Bus la kisasa ambalo hupeleka timu popote katika kushiriki katika mashindano mbalimbali,nategemea kwa siku za mbele KMC itacheza ligi kuu ya Tanzania Kwa hiyo vijana chezeni kwa Bidii mkijua kinondoni michezo inapewa kipaumbelee cha hali ya juu"Amesema Mstahiki Meya

Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Kinondoni Mh.Boniface Jacob akikabidhi kikombe kwa Nahonda wa shule ya sekondari Makongo .
No comments:
Post a Comment