Tuesday, 17 May 2016
MKUU MKOA WA DSM;Aelezea mchezo mchafu wa watumishi wa umma kuuza magari ya serikali............
Baadh wa watumishi wa umma wamekuwa wakifanya ujanja ujanja wa kuharibu magari ya serikali ili waweze kutengeneza mazingira ya kuyauza kwa watumishi wenyewe kwa wenyewe dani ya ofisi hiyo hiyo,akizungumza na wandishi wa habari mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul C Makonda wakati wa kutoa magari nane yaliyoenda kutengenezwa na umoja wa mafundi wa gereji wa wilaya ya kinondoni ikiwa ni kujitolea ili watumishi wa umma waweze kutekeleza majukumu yao bila ya kuleta visingizio vya kukosa usafiri.
Makonda amesema kuwa gari zinaharibika kitu kidogo lakini hayatengenezwi kwa muda muafaka na kufanya gari hizo kuharibiki wakati zikiwa zimeegeshwa na baadae kufanya mnada wakiwa wanunuzi wa gari hizo ni watumishi wa umma.
Amesema kuwa kwa wakati gari yoyote iliyotengenezwa na umoja huo ikiharibika tena basi dereva aliyeharibu atawajibika kwa kukatwa mshahara kwa ajili ya matengenezo ya gari hiyo.
Aidha,Amesema watumishi wa umma wanashindwa kuwatembelea wananchi kutokana na kukosa usafiri wakati magari yamekaa kwa muda mrefu na kuendeea kuharibika,Naye katibu mkuu wa umoja huo Abdallah Rashid amesema kuwa wataendelea kutoa ushirikiano na mkuu wa mkoa katika kuhakikisha magari yanakuwepo vizuri ili watumishi wa umma waweze kuwatembelea wananchi kujua matatizo yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment