Wednesday, 18 May 2016

MICHEZO:Yanga kuingia uwanjani leo kucheza na waangalo................

Image result for picha ya yanga
Kikosi cha timu ya Yanga kimefanya mazoezi mepesi mepesi leo  asubuhi ambayo ni mazoezi ya mwisho kuelekea mchezo wao wa marudiano wa kombe la shirikisho  afrika dhidi ya Gd Sagrada Esperanca nchini angola.
Yanga imewasili salama mjini Dundo,Angola juzi jioni baada ya safari ya kutwa nzima huku wachezaji wakionekana kupata usumbufu wa kubadilisha usafiri pamoja na baadhi yao kupoteza mabegi.
Meneja wa timu Hafidhi Salehe amesema kikosi kipo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo dhidi ya  wenyeji ambapo anajua mchezo huo utakuwa mgumu sana kwao,Amesema wachezaji wamefanya mazoezi ya mwisho(mepesi mepesi)leo asubuhi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa jioni,
"wachezaji wote wamefanya mazoezi ya mwisho lakini leo asubuhi wamefanya yale mepesi mepesi kuelekea mchezo jioni ambao ni muhimu sana kwetu"amesema Swalleh
Salleh  amesema wanatarajia leo jioni wanahakikisha watapata ushindi hasa baada ya wachezaji wao wawili ambao hawakucheza kwenye mechi ya jijini Dar es salaam watakuwemo kwa ajili ya kuongeza nguvu "Ngoma na Kamosoku wamejumuika katika kuelekea mchezo huu hasa baada ya ule wa awali kuwepo jukwani wakiwa wanatumikia adhabu ya  kadi za njano walozozipata kwenye mchezo wa Al-ahly"amesema Swalleh
Swalleh pia amemalizia kwa kusema hali za wachezaji wote zipo vizuri na wamejiandaa kuweza kushinda mchezo huo ambao ni muhimu sana kwao na kama watafanikiwa kushinda bhasi watasonga mpaka hatua ya makundi ya kombe la shirikisho afrika.

No comments:

Post a Comment