Friday, 20 May 2016

SERIKALI:Makamu wa rais azindua ripoti toleo la nane kuhusu hali ya uchumi Tanzania leo Dar es salaam..................


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano ya Tanzania Samia Hassan Suluhu akizungumza kwenye uzindunzi wa Ripoti ya toleo la nane kuhusu hali ya uchumi Tanzania iliyofanyika leo tarehe 20/05/2016 katika Hotel ya Hyatt Regency ,Jijini Dar es salaam.

 e
Baadhi wa washiriki wakimsikiliza makamu wa Rais wakati wa uzindunzi wa Ripoti ya toleo la nane ya hali ya uchumi Tanzania



Makamu wa Rais wa Jamhuri wa muungano ya Tanzania Samia hassan Suluhu akizungumza na  mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia Madame Bella Bird baada ya uzindunzi wa ripoti toleo la nane ya hali ya uchumi Tanzania.
Serikali imesisitiza azma yake  ya kuweka mazingira mazuri ya biashara ili kuwezesha sekta binafsi kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.Hali ya uchumi  Tanzania ni ripoti iliyochapishwa na  Benki ya dunia mara mbili kwa mwaka kwa lengo la kukuza mjadala wa sera inayojengeka baina ya wadau na watunga sera na kuchochea mdahalo kwenye masuala muhimu ya uchumi nchini.

No comments:

Post a Comment