Thursday, 19 May 2016

HABARI KUTOKA MIKOANI NYANDA ZA JUU:Mauaji msikiti wa Mwanza..................

Image result for ACP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa MwanzaImage result for ACP Ahmed Msangi, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza
Picha zikimuaonesha ACP Ahmedi Msangi ,Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mwanza.
Ndani ya msikiti wa Rahma "masjida Rahma" mkoani Mwanza mauaji yametokea watu watatu(3) waumini wa msikiti huo wamepoteza maisha;Watu waliouwawa katika tukio hilo ni Feroz Elias,Imamu wa msikiti Huo Mbwana Rajab na Khamisi Mponda ambaye ni Dereva wa Bodaboda,aliyejeuriwa ni Ismail Abeid mwanafunzi wa shule ya kiislamu ya Jabar iliyopo Nyasaka Jijini humo.
Tukio hilo limetokea usiku wa kuhamkia leo saa 02:30 usiku wakati waumini wa msikiti huo wakiendelea na swala ya insha,Wakati wa swala hiyo ikiendelea ghafla kundi kundi hilo la watu waliingia hapo na kuanza kuhoji "Kwa nini mnaswali wakati wenzetu wamekamatwa na wanashikiliwa na polisi"kauli ambayo iliambatana na mashambulizi.Mashuhuda wa tukio hilo ambao hawakutaka majina yao kutajwa(yamehifadhiwa)wamesema kuwa yawezekana chanzo cha mauaji hayo kinatokana na kuwepo kwa misikiti miwili ambayo ina uhasama wa muda mrefu.....shuhuda mmoja amesema "unajua katika eneo hili kuna misikiti miwiliambayo ina uhasama wa muda mrefuhili ndilo linaweza kuwa ndio tatizo"
Ameongezea kwa kusema"misikiti hii kama unavyoona ipo katika pori na ipo nje ya jiji na wakati wanatekeleza mauaji hayo walikuwa hawana hofu,suala linatupa wasiwasi mkubwa sana waumini"Shuhuda huyo alisema kwamba wauaji hao walikuwa na silaha za moto aina za SMG pamoja na mabomu ya moto ya kutengeneza na kwamba waliyarusha mabomu hayo lakini hayakuleta madhara yoyote.
Shekhe Hussein Ibrahim,Mwenyekiti wa baraza kuu la waislamu Tanzania (BAKWATA)wilaya ya Nyamagana amelaani kitendo hicho amesema kwamba vitendo vya namna hiyo havikubaliki katika dini ya kiislamu na kwamba waislamu wote wanapaswa kulaani matukio ya namna hiyo "Nilipata taarifa saa tatu usiku na niliondoka na nilipofika eneo la tukio nilikutana na watu watatu waliokuwa wamejeuriwa na watu waliokuwa wamekufa tukawachukua na kuwapeleka Bugando(hospitali ya Rufaa ya Bugando)kwa ajili ya kufanya Uchungunzi zaidi"amesema shekhe Hussein
Ahmed Msangi kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Kamishina msaidizi wa Polisi(SACP) wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo amesema kwamba katika tukio hilo watu watatu wanashikiliwa na polisi mkoani humo kwa ajili ya mahojiano"Polisi hivi sasa tunaendelea na upelelezi wa Tukio hilo na ninawaomba wananchi wawe watulivu katika kipindi hiki,polisi tunaendelea kuchunguza na pindi tutakapomaliza tutatoa taarifa kamili"amesema Kamanda Msangi

No comments:

Post a Comment