Saturday, 14 May 2016

AFYA:WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI 71 WAFANYIWA UCHUNGUZI WA KINYWA NA MENO BURE KLINIKI YA ABC,DAR ES SALAAM

 Mkuruzenzi wa Kliniki ya Meno ya ABC ya Jijini Dar es Salama, Dr. Gombo Felician (kulia) akizungumza na wanafunzi wapatao (71) wa  Shule ya Msingi Fedha ya Kawe, kabla ya kufanyiwa uchunguzi wa Afya ya Kinywa na Meno bure , ikiwa ni moja ya wanafunzi hao kutembelea kliniki hiyo kwa  kujifunza jinsi ya utunzaji wa kinywa na meno na kuwapa hamasa ya kupenda Udaktari na kati ya  wanafunzi 71, wanafunzi 45 wamekutwa na matatizo ya kinywa na wengine meno yamezibwa. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Mmoja wa wanafunzi hao akifanyiwa uchunguzi wa Kinywa na Meno
 Rehema Mgaya, ambae ni Mwalimu alieongozana na wanafunzi hao akifanyiwa uchunguzi wa kinywa na Meno ambapo amefurahishwa na huduma hiyo na kuwaomba waalimu wengine na Taasisi kuwapeleka wanafunzi na hata wafanyakazi kufanya uchunguzi kila mara wa Afya ya Kinywa na Meno kwa kutembelea Kliniki hiyo


 Mwalimu alie ongozana na wanafunzi hao alipata matukio wakati wanafunzi hao walipotembelea Kliniki ya ABC iliyopo, Msasani Jengo la Mgahawa wa KFC
 Wanafunzi hao wakifurahia jambo baada ya kufanyiwa uchunguzi wa Kinywa na Meno katika Kliniki ya ABC iliyopo Msasani Jijini Dar es Salaam
 Dr. Gombo akiagana na Wanafunzi kwa staili ya pekee huku wakiwa na tabasamu ya furaha wanafunzi hao

No comments:

Post a Comment