Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto), Flaviana Matata na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba wakiweka shada la maua kwenye kaburi la pamoja ikiwa sehemu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kumbukumbu ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye pamoaja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano January Makamba wakijiandaa kuwasha mishumaa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kushoto) akiweka mshumaa kwenye kaburi pamoja na Flaviana Matata kwenye maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa MV. Bukoba ambapo mamia ya watu walipoteza maisha.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye(kulia) akimsikiliza Flaviana Matata muda mfupi kabla ya kupiga picha ya pamoja za kumbukumbu ya maadhimisho ya miaka 20 ya kuzama kwa meli ya MV. Bukoba.
Picha ya Pamoja.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye akizungumza wakati wa kuangalia mazoezi ya uokoaji majini yaliyofanywa na vijana 50 waliohitimu mafunzo ya uokoaji yaliyodhaminiwa na Flaviana Matata Foundation pamoja na UTT wakati wa maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 20 tangia kuzama kwa meli ya MV. Bukoba yaliyofanyika mjini Mwanza ambapo mamia ya watu walifariki akiwemo mama mzazi na binamu wa Flaviana Matata.
Sehemu ya waliofuzu mafunzo ya uokoaji wakionyesha namna ya kuokoa watu majini wakishuhudiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, Mhe. January Makamba Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula na Flaviana Matata
Sehemu ya makaburi ya pamoja ya waliofariki kwenye ajali ya MV. Bukoba mwaka 1996 ambapo leo imetimia miaka 20 tangia ajali hiyo imetokea.
Viongozi wa Dini walioshiriki kwenye kutoa ibada maalum ya kumbukumbu ya miaka 20 tangia kutokea kwa ajali ya MV. Bukoba
No comments:
Post a Comment