SERIKALI kupitia wakala ya Serikali mtandao imesema kuwa inaendelea kulifanyia kazi suala la uanzishaji wa mfumo wa TEHAMA utakaowawezesha wananchi kupata huduma na taarifa mbalimbali za Serikali kupitia simu zao mkononi mahali popote walipo kwa njia ya mtandao.
Utaratibu huo pia utawawezesha wahitimu wa vyuo mbalimbali vya elimu nchini Tanzania kupata taarifa za ajira za Serikali na kuwawezesha kuomba nafasi hizo, kufuatilia majibu ya usaili walioufanya na kupata taarifa za kuitwa kazini kupitia namba za utambulisho watakazopewa kupitia ujumbe mfupi (sms).
Akizungumza na Wahariri wa vyombo vya Habari leo jijini Dar es salaam Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Serikali Mtandao (e-Government Agency) Dkt. Jabiri Bakari amesema kuwa mfumo huo utamuwezesha mwananchi kupata huduma za Serikali mahali popote alipo kufuatia mifumo ya TEHAMA kuwasiliana na kubadilishana taarifa.
Amesema kuwa dhana ya Serikali Mtandao ni kuwa na matumizi ya TEHAMA kwenye shughuli zote za Serikali kwa lengo la kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji kwenye huduma za Afya, Utalii, Malipo ya tozo za huduma,vibali, leseni ,elimu na huduma mbalimbali za Serikali.
Dkt. Jabiri amesema moja ya vitu vinavyosababisha usumbufu kwa wananchi kutokana na kukosekana kwa Serikali mtandao ni pale wanapohitaji kupata huduma za Serikali ikiwemo Hati ya kusafiria ambapo hulazimika kwenda Idara ya Uhamiaji kujaza fomu maalum na kisha kusubiri kwa muda wa zaidi ya wiki moja ili taarifa zao ziweze kuhakikiwa na taasisi nyingine za Serikali wakati suala hilo lingeweza kuchukua siku moja.
“Matumizi ya TEHAMA kwenye shughuli za Serikali hurahisiaha sana upatikanaji wa taarifa kwa kuwa mifumo inawasiliana na kubadilishana taarifa haimlazimu mwananchi kwenda kwenye taasisi zaidi ya tano kupata huduma yake” Amesisitiza Dkt. Jabiri.
Amesema taasisi za Serikali kama Jeshi la Polisi, Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Idara ya Uhamiaji, RITA na taasisi nyingine ambazo majukumu yao hutegemeana kupitia serikali mtandaomifumo ya taasisi hizo huunganishwa ili ifanye kazi pamoja kwa lengo la kuruhusu mifumo kuzungumza kumuhudumia mwanachi bila yeye kulazimia kuzifuata taasisi hizo.
Amesema kuwa pamoja na maboresho mbalimbali yanayoendelea ndani ya Serikali ya kujenga Serikali mtandao imara mfumo uliopo sasa kwenye baadhi ya taasisi humfanya mwananchi achukue muda mrefu kupata huduma.
Ameeleza kuwa taasisi za Serikali zinazofanya kazi katika mazingira yanayofanana zinaposhirikiana katika kutoa huduma Kupitia Serikali mtandao mwananchi wa kawaida hatajua nini kinaendelea, atakachokipata mwisho ni majibu ya huduma aliyoiomba kama ni Bandarini atachukua mzigo bila usumbufu wowote kwa kuwa suala la kodi, upakuaji na upakiaji wa mizigo na ukaguzi halitamgusa mwananchi.
Ameongeza kuwa ili Serikali mtandao iweze kufanya kazi yake ipasavyo nchini lazima kuwe na miundombinu ndani ya taasisi au nje pia uwepo wa mifumo Tumizi ( Application Systems) inayoshughulikia masuala mbalimbali, wafanyakazi pamoja na Sera, miongozo na taratibu za kusimamia TEHAMA kuwezesha huduma mtandao ( e - Servieces).
Dkt. Jabiri amesisitiza Tanzania iko kwenye hatua ya kwanza na ya pili, kwa maana ya taasisi nyingi za Serikali zina tovuti zenye taarifa za awali za kumsaidia mtu kujua nini kinapatikana au kutolewa na taasisi za serikali ili aweze kuchukua hatua ya kupata huduma.
Amesema Wakala ya Serikali mtandao imefanikiwa kuweka mifumo kwa maana ya Tovuti kuu ya Serikali, Tovuti ya Wananchi, Tovuti ya data huria ambayo ina taarifa mbalimbali za wananchi kuhusu Maji, Barua pepe ya Serikali (GMS) ambayo sasa inatumiwa na jumla ya taasisi 117 za Serikali na Balozi mbalimbali kwa lengo kuepuka matumizi ya barua pepe za muda.
Amebainisha kuwa Wakala ya Serikali Mtandao kwa sasa eGA katika awamu ya kwanza imeziuganisha taasisi 75 za serikali na Wizara zote za Serikali kupitia mkongo wa taifa, pia Wakala imeziunganisha Taasisi 72 zilizounganishwa kwa simu zinazotumia itifaki ya Intaneti kwenye mkongo wa taifa ili kurahisisha mawasiliano na kupunguza gharama.
Akijibu Suala la baadhi ya Taasisi za serikali kukawia kuunganishwa kwenye mtandao amesema kuwa awali hakukuwa na mfumo huo kutokana na baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye Sera, miongozo na taratibu zinazosimamia utendaji wa shughuli za kila siku serikali lakini sasa kuna mwongozo wa taasisi kuzingatia ili kuhakikisha mifumo ya taasisi za Serikali inawasiliana ili kufanya kazi pamoja kuondoa mapungufu yaliyokuwepo.
Aidha, mifumo ya utendaji kazi inabadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea kwenye taasisi hizo na kuongeza kuwa Wakala ya Serikali mtandao imekuwa makini sana kuhakikisha hakuna mfumo unaoinuka dhidi ya mwingine lengo likiwa kumhakikishia mwananchi kupata huduma katika eneo moja kwa muda mfupi.
Kwa upande wake Meneja Habari,Elimu na Mawasiliano wa Wakala hiyo Bi. Suzan Mshakangoto amesema kuwa suala la matumizi ya mitandao mbalimbali isiyo rasmi katika shughuli za serikali linafanyiwa kazi huku akisisitiza kwamba utaratibu unaandali wa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote ya matumizi ya barua pepe nje ya zile za serikali kwenye ofisi za umma yanafungwa kuanzia Saa 1:30 hadi saa 9:30.
Kwa sasa ni taasisi 72 tu za serikali zikiwemo Wizara zote, Wakala, Bunge na taasisi zimeunganishw, Aidha halmashauri 77 zimeunganishwa na mkongo wa taifa na kazi ya kuzifikia taasisi zote 500 inaendelea ili kuwezesha zoezi la kufunga huduma za mawasiliano za serikali nje ya mkongo wa taifa.
Takribani taasisi 200 za umma zina tovuti ili kurahisisha upatikanaji wataarifa na huduma kwa wananchi. Changamoto iliyopo ni Tovuti nyingi kukosa taarifa zilizohuishwa pia kuunganisha maeneo ambayo bado hayajafikiwa hasa Halmashsuri na vijiji ili kuwezesha taarifa mbalimbali kupatikana kwa wakati.
Wakala imepata mafanikio katika utekelezaji wa jitihada za Serikali mtandao hasa katika uwekaji wa mifumo ya Serikali kwa maana ya Tovuti kuu ya Serikali, Tovuti ya Wananchi, Tovuti ya data huria ambayo ina taarifa mbalimbali za wananchi kuhusu Maji, Barua pepe za Serikali ambayo sasa ina taasisi 117 na Balozi mbalimbali zinatumia GMS ili kuepuka matumizi ya barua pepe za muda.
Wakala ya Serikali Mtandao katika awamu ya kwanza imeunganisha taasisi 72 za serikali na Wizara zote za Serikali kupitia mkongo wa taifa pia imeziunganisha taasisi hizo na simu zinazotumia itifaki ya intaneti kwenye mkongo wa taifa ili kurahisisha mawasiliano na kupunguza gharama.
Akifafanua kuhusu hatua ya mifumo ya serikali kuchelewa kufanya kazi pamoja amesema hapo awali hakukuwa na mfumo uliowezesha jambo hilo kufanyika kutokana na baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza kwenye Sera, miongozo na taratibu zinazosimamia masuala ya TEHAMA nchini lakini sasa kuna mwongozo uliotolewa kuhakikisha mifumo ya taasisi za Serikali inawasiliana na kufanya kazi pamoja ili kuondoa mapungufu yaliyokuwepo.
Aidha, mifumo ya utendaji kazi inabadilika kulingana na mabadiliko yanayotokea kwenye taasisi hizo na kuongeza kuwa Wakala ya Serikali mtandao imekuwa makini sana kuhakikisha hakuna mfumo unaoinuka dhidi ya mwingine lengo likiwa kumhakikishia mwananchi kupata huduma katika eneo moja kwa muda mfupi.
Meneja Habari, Mawasiliano Suzan Mshekangoto amesema suala la matumizi ya mitandao mbalimbali isiyo rasmi katika shughuli za serikali linafanyiwa kazi huku akisisitiza kwamba utaratibu unaandaliwa kuhakikisha kuwa mawasiliano yote ya matumizi ya barua pepe nje ya zile za serikali kwenye ofisi za umma yanafungwa kuanzia Saa 1:30 hadi saa 9:30 alasiri.
Amefafanua kuwa taasisi 72 za serikali zikiwemo Wizara zote, Wakala, Bunge na Mahakama zimeunganishwa, Aidha halmashauri 77 zimeunganishwa na mkongo wa taifa na kazi ya kuzifikia zilizobaki inaendelea ili kuwezesha mawasiliano ya serikali kupita kwenye mkongo wa taifa.
Bi. Suzan amesema mpaka sasa takribani taasisi 200 za umma zina tovuti zenye taarifa za huduma mbalimbali zinazotolewa na Serikali huku Changamoto iliyopo ni baadhi ya Tovuti hizo kukosa taarifa zilizohuishwa.
No comments:
Post a Comment