Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es salaam,Chamuriho amesema kuwa mtambo huo ni lazima uangaliwe kwa umakini kutokana na serikali ndipo inapata kodihalisi ya mafuta yanayoshushwa na meli.....amesema mkandarasi msambazaji wa vifaa kutokana na mkataba ni lazima ahakikishe kwa vitu vilivyopata kasoro kutatua kabla ya tatizo halijawa kubwa au kutojirudia tena.
Aidha amesema kuwa sauala la kamera ambazo zimepata hitilafu baada ya kupigwa na radi zitengenezwe mara moja na tatizo lisijirudie wakati mwingine kutokana na umuhimu wa kamera eneo hilo.
Amesema kutokana na hali hiyoamemtaka kaimu meneja wa Bandarikupeleka taarifa jumatatuikiwa ina vitu vyote ambavyo vipo katika mradi wa mtambo huo.....Naye Menaja wa mradi wa kupima mafuta Mhandisi Marry Mhayaya amesema kuwa jana kumetokea na changamoto katika mtamboiliyotokana na mafuta kukwama na kutoka na uchafu ambapo wameweza kusafisha.....Aidha amesema katika majaribio wa mtambo huo umeweza kuwa na mafanikio baada ya meli tatu kushusha mafuta bila ya matatizo yoyote.
Katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi na mawasiliano muhandisi Dr Leonard chamuriho akipa maelekezo kwa meneja wa matambo wa kupima mafuta (TPA) muhandisi Marry mhayaya leo baada ya katibu mkuu kufanya ziara ya kushtukiza kigamboni jijini Dar es salaam.
Katibu mkuu wa wizara ya uchukuzi,ujenzi na mawasiliano-uchukuzi muhandisi Dr Leonard Chimuriho akiwa juu ya mtambo wa mafuta akiangalia miundo mbinu yake wakati wa ziara yake ya kushtukiza kigamboni jijini Dar es salaam.
Mtambo wa kupima mafuta kigamboni jijini Dar es salaam
Mtambo wa kupima mafuta kigamboni jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment