Monday, 1 August 2016

MP IN KIBAHA:MBUNGE WA KIBAHA VIJIJINI AKABIDHI MADAWATI 537 NA VITABU KWA UONGOZI WA HALMASHAURI

kibah1Baadhi ya walimu,madiwani, watendaji wa serikali wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa halfa fupi ya ugawaji wa madawati pamoja na vitabu sherehe zilizofanyika kwenye shule ya sekondari Kilinaga langa.kibh2Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini Hamoud Juma wa kulia akimkabidhi madawati 537  Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibaha vijijini Mansouri Kisebengo katika sherehe ya makabidhiano iliyofanyika katika shule ya sekondari kilanga langa(PICHA ZOTE  NA VICTOR MASANGU)
………………………………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA  
WANAFUNZI wa shule za msingi na sekondari katika halmashauri ya Kibaha Vijijini  Mkoa wa Pwani waliokuwa wanakabiliwa na chanagamoto ya uhaba wa madawati na viti na kusababisha baadhi yao kuwa tabia ya utoro kwa sasa wameanza kunufaika na agizo la Rais Dr.John Magufuli la kutaka wanafunzi wote nchini kuhakikisha wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati.
Agizo hilo la Rais limetekelezwa  na Mbunge wa Jimbo la Kibaha Vijijini Hamoud  Jumaa kupitia kupitia fedha ambazo zimepatikana kutokana na kubana matumizi yasiyo ya lazima katika ofisi yake kwa lengo la kuweza kusaidia katika kuboresha sekta ya elimu.
Akikabidhi jumla ya  madawati 537 Mbunge wa Jimbo hilo kwa uongozi wa halmashauri ya kibaha vijijini katika halfa fupi zilizofanyika katika shule ya sekondari kilangalanga iliyopo Mlandizi, amesema kwamba ametoa  madawati hao pamoja na vitabu kwa lengo la kuweza kupunguza kero  na kuondokana na adha  ambayo walikuwa wanaipata wanafunzi wa jimbo lake katika siku za nyuma.
Kwa upande wake Afisa elimu katika halmashauri ya kibaha vijijini Coskansia Mafuru amebainisha kwamba awali kabla ya agizo la Rais walikuwa wana upungufu wa madawati 1923 kwa shule za msingi, hivyo msaada huo utaweza kumaliza changamoto zilizokuwa zikiwakabili na kuongeza kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Alisema kwamba kukamilisha agizo ambalo limetolewa na rais litaweza kuwa ni mkombozi mkubwa sana kwa wanafunzi na wataweza kuongeza kasi ya ufaulu kwani hapo awali walikuwa wanasoma katika mazingira ambayo sio rafiki kwao na wengine kusoma wakiwa wamekaa chini.
“Katika kukamilisha zoezi hili na agizo lililotolewa na Rais kuhakikisha kwamba tunafanya kila jitihada ili kuweza kuhakikisha wote wanasoma wakiwa wamekaa kwenye madawati na sio chini hivyo madawati hayo yametokana na kubana matumizi mbali mbali katika ofisi ya Mbunge hivyo nina imani ni moja ya hatua nzuri katika kuendelea kuboresha sekta ya elimu katika jimbo langu,”alisema Jumaa.
Pia alisema kwamba pamoja na agioz hilo pia ataendelea kujitahidi kushirikiana na wa madiwani wote katika halmashauri ya Kibaha vijiji pamoja na wadau wengine ili kuweza kuendeleza kutoa sapoti katika kununua mahitaji mengine muhimu ikiwemo vitabu ambavyo viyaweza kuwapa fursa wanafunzi kuweza kujisomea.
Naye Mkuu wa shule ya sekondari Kilangalanga Albert Mabiki, pamoja na Mwenyekiti wa halmashauri ya Kibaha vijijini Mansouri Kisebengo hapa wanazungumza changamoto zilizokuwa zinawakabili wanafunzi pamoja na kushindwa kufanya vizuri kutokana na kuwepo kwa mlundikano mkubwa wa wanafunzi pamoja na hali ya kuwepo kwa  utoro.
“Ni kweli changamoto ya watoto wetu walikuwa wanasoma katika mazingira ya mlundikano, na wakati mwingine baadhi ya wanafunzi wanakuwa ni watoro hawafiki shuleni nah ii ni kutokana na kutokuwepo kwa madawati na viti vya kutosha lakini kwa hali hii na agizo la Rais wetu hakika kwa sasa hata huu utoro utamalizika katika baadhi ya maeneo.
MADAWATI hayo pamoja na vitabu  ambayo vimetolewa  na ofisi ya Mbunge wa jimbo la Kibaha vijijini vimegharimu  kiasi cha  zaidi ya shilingi  milioni 100 ambapo kata zote 14 ambapo kuna shule za msingi na sekondari zimeweza kupatiwa mgao huo kwa baadhi ya shulezenye mahitaji makubwa  kwa ajili ya kuweza kutekeleza agizo lililotolewa na Rais.

No comments:

Post a Comment