Saturday, 4 June 2016
HALMASHAURI YA KINONDONI:Watu 49 wamekamatwa kwa kutumia vyombo vya moto katika miundo mbinu ya DART-Hapi
Mkuu wa wilaya ya kinondoni Salum Hapi akizungumza na waandishi wa Habari juu ya wananchi wa kinondoni kufuata sheria katika Barabara ya mabasi yaendayo haraka...pembeni aliyekaa ni Mstahiki Meya wa halmashauri ya Kinondoni Mh.Boniface Jacob
Baadhi ya wananchi na waandishi wa habari wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh. Salum Hapi.
Mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh. Salum Hapi amewataka wananchi wa kinondoni kufuata sheria katika Barabara ya mabasi yaendayo haraka,Hapi ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utekelezaji wa agizo la Rais,Amesema watu 49 wamekamatwa ambao wamekuwa wakitumia vyombo vya moto katika barabara ya mwendokasi,Hapi amesema kuwa Barabara hiyo watu waheshimu sheria za nchi na watu watakaokiuka watachukuliwa hatua za kisheria,Aidha amewataka DART kuongeza ukaguzi wa abiria katika vituo vyake kwani sio watu wote wanasafiri wengine ni waharifu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment