Wednesday, 8 June 2016

SIASA:UKAWA WAKIMCHAFUA DK.MAGUFULI TUTAKULA NAO SAHANI MOJA KUMTETEA







NA BASHIR NKOROMO
CHAMA
Cha Mapinduzi (CCM),  kimeonya  vikali
juu ya  mkakati wa  viongozi wa UKAWA,  wa kufanya ziara   mikoani, katika kile ambacho wanakiita ni
kwenda kuishitaka serikali  ya awamu ya
tano  chini ya  Rais Dk. John Magufuli  kwa wananchi.
 
Aidha
CCM  kimesema, daima hakitavumilia  juu ya jambo lolote  ambalo litaonekana kuwa na nia ovu ya
kumchafua Rais Dk. Mafuli  na  kitakula sahani moja  na UKAWA  katika kampeni hiyo.
 
Akizungumza
na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, jana, Msemaji wa CCM, Christopher
Ole Sendeka, alisema, wamesikitishwa  na
kauli  zinazotolewa na  wapinzani
ya kupinga  kasi ya Rais Dk.
Magufuli hususan katika dhama yake ya utumbuaji majipu, kubana bajeti na
matumizi ya serikali pamoja na  kuzitafutia ufumbuzi  changamoto za wananchi katika sekta
mbalimbali.
 
Sendeka
alisema, upo mkakati mchafu ambao wapinzani wamekuwa wakipanga  kwa nia mbaya ya kutaka kuchafua taswira ya
Rais Dk. Magufuli , mkakati  ambao  amedai  hauwezi kuungwa mkono na wananchi.
 
Alisema,
tangu Mei 16 mwaka huu baada  ya Kikao
cha Kamati Kuu ya CHADEMA, habari za mwanzo zilianza kuandikwa katika vyombo
mbalimbali vya habari juu ya yaliyojiri katika mkutano huo.
 
Alisema,   mkakati   huo
unaegemea katika kuandaa umma kwa kile kinachoitwa kwenda kumshitaki
Rais Dk. Magufuli kwa wananchi.
 
“Kwamba
Serikali ya  Rais Dk. Magufuli  inaidaiwa kuendesha nchi kifashist na
inalenga kuipeleka nchi  katika utawala  wa kidikteta ambao haujazoeleka katika nchi
yetu,”alisema Sendeka.
 
Alisema,
kipindi cha nyuma moja ya mambo ambayo yalikuwa yakipigiwa kelele na vyama
vyote ni ufisadi, rushwa  na  suala la
serikali kutokuwa na maamuzi, ambapo baada ya uchaguzi  mkuu uliopita,  baada ya Rais Dk. Magufuli kuchaguliwa  amesimama kidete kupambana na  mambo hayo licha ya kwamba   yapo katika, ilani ,  sera za msingi na  kiapo cha
uanachama cha CCM.

No comments:

Post a Comment