Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt John Pombe Magufuli amewataka wakuu wa wilaya na mikoa kuchapa kazi kwa bidii kwani viongozi hao ndio wawakilishi wa wananchi wa vijijini.
Mhe.Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizungumza wakati wakuu wa wilaya na mikoa walipokuwa Ikulu wakila kiapo cha maadili ya viongozi kabla ya kwenda kuapishwa na wakuu wa mikoa yao.
Rais Magufuli pia amewataka viongozi hao kufanya kazi na kutimiza majukumu yao kwani wananchi wana changamoto nyingi,na wao waende kutatua matatizo ya wananchi walio maskini.
Aidha amewataka viongozi hao kutokuwa chanzo cha kutengeneza matatizo katika jamii na hivyo wasimamie haki na ukweli,wasiwe wala rushwa,wazingatie maadili na kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi za vyama zao,dini au kabila uku akiwataka kutekeleza waliyohaidi kwenye ilani ya chama cha mapinduzi.
Pia amewataka viongozi hao kuweke mkazo katika kutatua kero za wananchi na kuwataka kutimiza kwa vitendo kwa kushirikiana na viongozi watakaowakuta katika maeneo yao waliyopangiwa.
Hata hivyo amewataka viongozi hao kusimamia mapato ya Serikali katika miradi yote kwenye maeneo yao ili kuhakikisha serikali inapata kodi ambayo itasaidia katika maendeleo ya Taifa hili.
No comments:
Post a Comment