Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia) akizungumza na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa tatu kutoka kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Comoro Mhe.Azali Assouman na ujumbe wake walipokutana kwenye uwanja wa ndege wa Dar es Salaam ambapo Rais huyo wa Comoro alikuwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari ya kwenda Macca kwenye ibada ya Umrah nchini Saudi Arabia.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo Balozi wa Japan Nchini alisema nchi yake imeridhishwa na kasi ya Serikali ya Rais Mhe. Magufuli na kuahidi kuendelea kuisaidia Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa
kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu mara
baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Japan nchini Mhe. Yoshida Masaharu mara
baada ya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam.
………………………………………………
Rais wa Comoro AzaliI Assouman amesema serikali yake itaendelea kudumisha uhusianona ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Comoro katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya na biashara.
Rais huyo wa Comoro ametoa kauli hiyo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa niaba ya Rais John Pombe Magufuli akiwa kwenye mapumziko mafupi kabla ya kuendelea na safari yake ya Mecca – Saudi
Arabia kwa ajili ya ibada ya UMRAH.RaisAzali Assouman pia amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya Tanozinazolenga kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii nakusisitiza kuwa serikali yake itaendelea kujifunza kutoka Tanzania ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Komoro.
Akitoa ujumbe wa Rais JOHN MAGUFULI kwa Rais wa Comoro Azali assouman, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amemhakikishia Rais wa Comoro kuwa Tanzania itadumisha uhusiano uliopo kati ya nchi hizo MBILI hasa kwenye sekta za elimu, afya na biashara kwa ajili ya manufaa ya nchi hizo MBILI.
Makamu wa Rais pia amemtakia Rais wa Comoro kheri katika safari yake ya Mecca– Saudi Arabia kwa ajili ya Ibada ya Umrah.
Wakati huo huo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa JAPAN hapa nchini Masaharu Yoshida na kumweleza kuwa serikali itaendelea kuweka na kuboresha mazingira bora kwa ajili ya wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo wawekezaji kutoka
nchini JAPAN.
nchini JAPAN.
Makamu wa Rais amesema serikali ya JAPAN imekuwa mshirika mkubwa wa maendeleo kwa Tanzania katika kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo Tanzania Bara na Visiwa hasa kwenye sekta ya elimu, afya na maji na kusema jambo hilo ni zuri na lakuigwa na washirika wengine wa maendeleo.
Kwa upande wake Balozi wa Japan hapa nchini MASAHARU YOSHINDA amemhakikishia Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN kuwa nchi yake itaendelea kufadhili ipasavyo miradi ya maendeleo hapa nchini ili kuhakikisha wananchi wa Tanzania wanapata huduma bora za kijamii.
No comments:
Post a Comment