Wednesday, 22 June 2016

PROF. MAKAME MBARAWA AZINDUA BODI YA TPA

TPA1Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka, akitoa ufafanuzi kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati), wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo jijini Dar es Salaam.Kulia ni Katibu MKuu wa WIzara hiyo, Sekta ya Uchukuzi, Dr. Leonard Chamuriho.
TPA2Wajumbe wa Bodi mpya ya Bandari Nchini (TPA), wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, wakati wa uzinduzi wa bodi hiyo.
TPA3Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka (kulia), akimkabidhi Mwenyekiti mpya wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka, vitendea kazi baada ya kuizindua rasmi bodi hiyo.
TPA4Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Hebel Mhanga alipokagua eneo la kupakulia makontena bandarini hapo.
TPA5Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini (TPA), Eng. Aloyce Matei (wa kwanza kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (wa pili kushoto), alipokagua miundombinu ya Bandari ya Dar es Salaam.
TPA6Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Profesa Ignas  Rubaratuka (kushoto), wakati alipokagua eneo la kuhifadhia  magari katika bandari ya Dar es Salaam.
Habari Picha na Benjamini Sawe-Maelezo.

No comments:

Post a Comment