Friday, 17 June 2016

MONTAGE LIMITED, SERENA NA NMB ZATOA MSAADA KWENYE KITUO CHA MTC BUNJU

1Bi. Teddy Mapunda Mkurugenzi wa Kampuni ya Montage Limited na Serafine Lusala Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya Serena wakishiriki kazi ya kupaka rangi kwenye jengo  linalotumiwa na wanafunzi wa kituo  cha mafunzo kwa vijana  cha Multpurpose Training Center kilichopo Bunju wilaya ya Kinondoni jijini Dar es salaam kwa ajili  ya kulia chakula jana, Kampuni za Montage Limited, Serena Hotel na Benki ya NMB ziliungana kwa pamoja na kukipa msaada wa vitu mbalimbali  ikiwemo rangi, madaftari, mafuta ya kupaka  chakula vifaa vingine  katika kituo hicho vyenye thamani ya shilingi milioni tano.2Serafine Lusala Mkurugenzi wa Masoko Hoteli ya Serena akipaka rangi kwenye ukuta wa jengo hilo huku wafanyakazi wenzake wakimuangalia.
3
Wafanyakazi wa Hoteli ya Serena wakishiriki kupaka rangi
4
Wafanyakzi wa Kampuni ya Montage wakishiriki kupaka rangi katika jengo hilo.
5
Mratibu wa kituo cha MTC Bw.Issa Buzohela akielezea jambo wakati ugeni huo ulipotembelea kwenye darasa la vijana wanaojifunza ufundi seremala kituoni hapo.
6
Hawa ni wanafunzi wanaojifunza kushona nguo kutuoni hapo wakiendelea na mafunzo.
7
Ugeni huo ukishuhudia jinsi wanafunzi hao wanavyojifunza kushona nguo.
8
Kituo hiki pia kinatoa mafunzo ya kuzima moto na uokoaji haoa wanafunzi wakiwa tayari wamevalia ngua maalum kwa ajili ya kuokoa mtu aliyenasa kwenye jengo refu linalowaka moto.
9
Nguzo hii ya chuma ni mfano wa jengo na mtu aliyenasa yuko juu hivyo wanafanya kazi ya kumuokoa.
10
Tayari wanamshusha kwa kutumia Machela, kamba, na ngazi kama inyoonekana katika picha 
11
Wanaendelea kushusha chini.
12Hapa tayari ameshaokolewa na taratibu zinazofuata sasa ni kumpa huduma ya kwanza na kisha kumpeleka hospitali.

No comments:

Post a Comment