Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. Katika tukio hilo Dk. Tulia Ackson alichangia kiasi cha shilingi milioni moja.
|
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto), Msanii wa Bongo Movie, Aunt Ezekiel (kulia) na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (katikati) wakiosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. |
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia) akiosha gari na Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kushoto) kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. Katika tukio hilo Dk. Hamisi Kigwangalla alichangia shilingi milioni moja. |
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla akiosha gari katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. |
|
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kulia) akiosha moja ya magari ya wabunge kuwaunga mkono waandishi wa habari katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. |
|
Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja (aliyeshika kipaza sauti) akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu na Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson (katikati). Katika zoezi hilo Ngeleja alichangia shilingi laki moja huku timu ya bunge ikichangia shs milioni moja. |
|
Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson (katikati) akizungumza katika zoezi la kuosha magari kwenye kampeni maalumu ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ ikiwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson na Mwenyekiti wa Bunge Sports, William Ngeleja (kushoto). |
|
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kulia) akizungumza kuwapongeza waandaaji wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’ asubuhi katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma. Dk. Tulia alichangia shs milioni tano. |
|
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Ackson Mwansasu (kushoto) akiosha moja ya magari ya wabunge kuwaunga mkono waandishi wa habari katika tukio la kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini tukio hilo lilifanyika jana katika Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma. |
|
Mmoja wa wasanii wa muziki akijitolea kuosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. |
|
Mmoja wa wasanii wa muziki akijitolea kuosha moja ya magari ya wabunge na wadau wengine kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. |
|
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati) akimkabidhi hudi ya shs milioni moja Mwenyekiti wa kampeni ya Okoa Maisha ya Waandishi wa Habari ‘Media Car Wash For Health’, Benjamin Thompson (kushoto) kwa ajili ya kuchangia fedha kuwakatia bima ya afya waandishi wa habari nchini. Kulia ni Mratibu wa zoezi hilo. |
|
Miss Tanzania 2014/15, Lilian Kamazima (kulia) na Mkurugenzi wa Utafiti na Masoko wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Athuman Rehani (kushoto) wakijitolea kuosha magari kwenye kampeni hizo. NHIF waliosha gari lao kwa shs 100,000/-.
…………………………………………………………………………….
Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson ameshiriki harambee ya kuchangia waandishi wa habari kwa ajili ya kuwakatia Bima ya Afya “Media Car Wash For Health” iliyofanyika leo katika viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma ambapo amechangia jumla ya shilingi milioni 5 ili kuokoa maisha ya waandishi wa habari.
“Kuna umuhimu mkubwa wa kuwachangia waandishi wa habari kwani wamekuwa na mchango mkubwa katika kuleta maendeleo ya nchi na kuhamasisha amani ya nchi, kwa kutambua umuhimu wao nitachangia shilingi 5,000,000 ili iweze kuwakatia Bima ya Afya,” alisema Mhe.Dkt. Tulia.
Licha ya kuchangia fedha hizo Mhe. Tulia aliosha baadhi ya magari ya waheshimiwa wabunge kwa ajili ya kuchangia harambee hiyo ambapo kila mbunge aliyeoshewa gari yake alichangia shilingi 100,000 ambazo moja kwa moja ziliingia katika mfuko wa kuokoa maisha ya waandishi wa habari kwa kuwakatia Bima ya Afya.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Maendelea ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Hamis Kigwangalla amechangia shilingi 1,000,000/= ambayo nayo inaenda kusaidia waandishi wa habari ili waweze kukatiwa Bima ya Afya.
Lengo la harambee hiyo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 200 ambazo zitatumika kuwakatia Bima ya afya zaidi ya waandishi wa habari 1000 hapa nchini. Aidha harambee hii ni ya pili, harambee nyingine kama hii ilifanyika mwaka 2015, viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam na kufanikiwa kukusanya shilingi milioni 30 ambazo zilisaidia kugharamia matibabu kwa waandishi watatu waliokuwa wanaugua kwa kipindi kirefu.
|
No comments:
Post a Comment