Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akipokea taarifa ya makabidhiano kutoka kwa aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (kushoto) pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto meza kuu) akimsikiliza aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga alipokuwa anazungumza na Waziri huyo pamoja na Watendaji Wakuu wa Wizara hiyo, kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo, mara baada ya Wizara Mwigulu kupokea taarifa ya makabidhiano ofisini humo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira (wa pili kulia) alipokuwa anazungumza kabla ya aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga (wa tatu kulia) kukabidhi ofisi kwa Waziri Mwigulu. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Balozi Simba Yahya. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
No comments:
Post a Comment