Saturday, 4 June 2016

MICHEZO:Misri yafuzu AFCON 2017 kwa kuifunga Taifa Stars 2-0



Kutoka kushoto Kocha mkuu wa Tanzania Taifa stars Charles Mkwasa,kocha Msaidizi Hemedi Morocco,Kocha wa Makipa Peter Manyika na Mkurugenzi wa Benchi la Ufundi Abdallah Kibadeni wakifatilia mchezo wa Taifa stars na Misri Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.


Mchezaji wa Timu ya Taifa stars(Tanzania) Juma Abduli akiwa kwenye harakati za kumuacha mchezaji wa Misri.




Mchezo ukiendelea akionekana Thomasi Ulimwengu aliyekuwa na mpira(Tanzania)pembeni wachezaji wa Misri wakimuangalia kwa makini.

Kocha mkuu wa kikosi cha Tanzania Taifa stars Charles Boniface Mkwasa amekubali matokea ya kufungwa goli 2-0 na Misri huku akisifia kikosi cha Misri ni kizuri na wana wachezaji wazuri na wanacheza kwa nidhamu ya hali ya juu,akizungumza baada ya mechi kumalizika Mkwasa amesema kwamba wachezaji wake wamecheza vizuri ila wameshindwa kuzitumia nafasi walizozipata kipindi cha kwanza na makosa madogo madogo kutoka kwa wachezaji na hasa goli la pili lilikuwa ni kosa la mabeki katika kufanya marking ya mwisho hata nawapongeza sana Misri kwani wamepata alama tatu na kuweza kufuzu mataifa Afrika 2017 nchini Gabon.Magoli ya Misri yote yamefungwa na Mohamed Salah anayecheza soka la kulipwa Italia timu ya Fiorentina.

No comments:

Post a Comment