Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika (hawapo pichani) walipomtembelea ofisini kwake kwa nia ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora (kulia) akimsikiliza Mkurugenzi mtendaji wa Kampuni ya Oracle Afrika Bw. Cherian Varghese (katikati) akielezea nia ya Kampuni yao katika ushirikiano wa kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA hapa nchini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia sekta ya Mawasiliano Dkt. Mhandisi Maria Sasabo (wa kwanza kushoto) akizungumza na ujumbe kutoka Kampuni ya Oracle Afrika walipotembelea sekta ya Mawasiliano na kueleza nia yao ya ushirikiano katika kulinda miundombinu na mifumo ya TEHAMA.
…………………………………………………………………………….
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Prof. Faustin Kamuzora amekutana na ujumbe wa Kampuni ya Oracle Sysytem Limited ambayo imeonesha nia na utayari wa kuwekeza kwenye Sekta ya Mawasiliano Tanzania
Kampuni ya Oracle Sytem Limited kwa kushirikiana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano itakuwa na mkutano wa The Africa Security Summit utakaofanyika hoteli ya Kilimanjaro, Dar es Salaam tarehe 30 Juni, 2016.
Lengo la mkutano huo ni kuwakutanisha wadau na wataalamu mbalimbli wa Taasisi za Serikali na sekta binafsi wapatao 200 kutoka ndani na nje ya nchi iki kuona namna wanavyoweza kuwekeza hapa nchini.
Hayo yameelezwa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Oracle system Ltd wa Kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Bwana Cherian Varghese, wakati akiongea na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Sekta ya Mawasiliano Prof. Faustin Kamuzora alipokutana na ujumbe wa Kampuni hiyo kuzungumza nae kuhusu maandalizi ya mkutano huo na nia yao ya kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendeleza Sekta ya Mawasiliano
Bwana Varghese amesema kuwa mkutano huo utawawezesha wataalamu wa watanzania na kuwajengea uwezo na kuongeza uelewa wa usalama wa taarifa na umuhimu wake na namna ya kuzitumia ili kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya Taifa la Tanzania. Pia Kampuni yake imetambua na kuona namna ambavyo Tanzania imewekeza na kuthamini Sekta ya Mawasilino kwa kuwa na miundombinu ya kisasa, Sera, sheria na kanuni zinazosimamia Sekta ya Mawasiliano na kutambua mchango wake katika kukuza uchumi.
Prof. Kamuzora aliwaahidi kuwa Wizara itawapatia ushirikiano wa kutosha ili Taifa liweze kunufaika kupitia utaalamu, ujuzi na weledi wa Kampuni ya Oracle ili kuendeleza Sekta ya Mawasiliano nchini
Kampuni hiyo tayari imewekeza na kushirikiana na nchi nyingine za Afrika ikiwemo Zambia, Zimbabwe, Afrika Kusini, Kenya na Uganda kuendeleza Sekta ya Mawasiliano katika maeneo ya usalama wa taarifa na kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa kutumia njia ya kielektroniki
No comments:
Post a Comment