Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema serikali yake itaendelea na mpango wa kuwahamishia Wayahudi wa Ethiopia hadi nchini Israel.
Amesema serikali yake itahakikisha Wayahudi waliokwama nchini Ethiopia wanasafiri kujiunga na jamaa zao ambao tayari wamefika Israel.
Takriban Waethiopia 9,000 wanaodai kuwa Wayahudi wanasubiri kuhamia Israel, na wamesubiri kwa miaka mingi.
Akihutubia wanahabari mjini Addis Ababa, bw Netanyahu amesema shughuli hiyo itatekelezwa hivi karibuni ingawa hakueleza ni wakati gani.
“Kuhusu kuwapeleka Israel watu wa jamii (Wayahudi Waethiopia) ambao bado wapo hapa, tunafanya hivyo, tuliahidi, na tutatimiza ahadi hiyo kwa ngazi ya utu kuhakikisha familia zinaungana tena,” amesema.
“Haitafanyika siku za baadaye, bali itafanyika sasa chini ya bajeti ya sasa. Tumejitolea katika mpango Fulani na tutaukamilisha.”.
Takriban Wayahudi Waethiopia 130,000 wanaishi Israel kwa sasa, tangu shughuli ya kuwahamisha ianze 1984.
Serikali ya Israel hata hivyo imeshutumiwa kwa kutohakikisha Wayahudi Waethiopia wanaingiana vyema na kukubalika katika jamii Ethiopia.
Miezi ya karibuni, mamia ya Wayahudi Waethiopia wameandamana Israel wakidai kubaguliwa.
No comments:
Post a Comment