Mkuu wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi akiongea na wakulima wadogowadogo
wanaosafirisha mazao yao ya chakula kutoka mashambani mwao wakati alipokutana
nao njiani akiwa katika ziara vijiji vya Kata ya Kagera Nkanda.

Mkuu wa Wilaya ya Kasulu, Kanali Martin Mkisi (mwenye sare za jeshi) akiongea na viongozi wa vijiji vvya Kagera Nkanda, na kutafuta ufumbuzi wa kero za wananchi katika vijiji vyao.
Viongozi wa vijiji vya Kata ya Kagera Nkanda, pamoja na wakuu wa idara mbalimbali wa
halmashauri ya Wilaya wa Kasulu, wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa wilaya.

***************
Na Father Kidevu Blog, Kasulu
MKUU wa Wiaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Kanali Martin Mkisi amepiga marufuku
usafirishaji wa mazao nyakati za usiku na kuagiza wakulima wadogo Wilayani humo
kutotozwa ushuru wa mazoa na badala yake ushuru huo utozwe kwa wakulima wakubwa
pekee.

Kanali Mkisi alitoa agizo hilo jana wakati akizungumza kwa nyakati tofauti alipofanya
ziara katika ya Kagera Nkanda na vijiji vyake kutatua kero hiyo ya ushuru wa
mazao iliyokuwa ikiwakabili wananchi wa maeneo hayo kwa muda mrefu.

Mkisi aliyeambatana na watendaji wengine wa serikali Wilayani humo, akiwepo
Mkurugenzi wa Hamashauri, Katibu Tawala Wilaya pamoja na Mwekahazina wa Wilaya na
maafisa wengine.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya ameagiza viongozi wa vijiji vyote kuweka utaratibu wa
kuwatambua wakulima wadogo katika maeneo yao ili kupata vibali
vitakavyowaruhusu kusafirisha mazao yao kutoka shambani hadi nyumbani bila
kulipa ushuru.

“Wakulima wadogo wote watambuliwe na serikali za vijiji ili kupata vibali
vitakavyowaruhusu kuondoa mazao yao mashambani bila kulipa ushuru, ni dhahiri
ushuru huu ni kero ya muda mrefu kwa wakulima hawa wadaogo ambao hulima mazao
yao ya chakula na si ya biashara,”alisema Kanali Mkisi.

Pia amewataka wakulima wakubwa wa kilimo cha biashara waishio mjini na kulima
vijiji vya Kagera Nkanda waendelee kutoa ushuru kwa mujibu wa sheria namba 9
kifungu cha 7 ya mapato ya mazao na kupiga marufuku usafirishaji wa mazao usiku.

Kanali Mkisi pia amewataka watendaji wa Vijiji kuboresha namna ya usimamizi na udhibiti
wa mapato na kuahidi kushirikiana nao katika kuboresha.

“Ninaamuru kwamba matumizi ya mapato lazima yaelekezwe kwenye huduma za kijamii,
maji,afya, elimu, miundombinu… hususan maboresho ya barabara korofi ya kutoka
Kasulu mjini hadi vijiji vya Kagera Nkanda ambayo tayari ina mkandarasi
kwaajili ya matengenezo,”aliongeza Kanali Mkisi.

Mkisi pia ameagiza mazingira ya kufanyia kazi kwa wakusanya ushuru wa mazao na mapato
mengine kuboreshwa mara moja huku akiagiza wataalam wa kodi kufika maeneo yote
ya vijijini na kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa wananchi.

Kero ya wakulima wadogo kutozwa ushuru wa mazao watokapo kuvuna mazao yao hasa
katika vijiji viliovyopo katika Kata ya Kagera Nkanda ilikuwa ni ya muda mrefu
na imekuwa ikileta usumbufu kwa wananchi.

No comments:
Post a Comment