Na Abdulaziz Video,Lindi
Shule ya Sekondari ya Lindi imeteketea kwa moto usiku wa kuamkia leo. Moto huo ambao ulianza majira ya saa saba usiku na Uliweza Kudhibitiwa kutoleta Athari zaidi baada ya Jeshi la Polisi, Kikosi cha Zimamoto na Wananchi kushirikiana kwa pamoja na kufanikiwa kuudhibiti saa Moja asubuhi ya leo.
Moto ukiendelea kuwaka katika moja ya majengo ya Shule hiyo.
Mpaka moto huu ulipodhibitiwa mali zifuatazo zilikuwa tayari zimeshaungua:-
• Madarasa tisa yameungua, ambapo matano yameungua pamoja na samani zilizokuwa ndani na mengine manne ni majengo peke yake Vifaa viliwahi kuokolewa na wananchi.
• Ofisi nne za walimu.
• Maabara mbili za kemia na fizikia zimeungua kwenye paa tu, hivyo samani za ndani hazijaungua.
• Takribani madawati zaidi ya 300 yameteketea kwa moto.
Majengo mengine ya shule yapo salama yakiwemo mabweni.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi amewaomba wananchi na uongozi wa shule kuwa watulivu wakati Uongozi wa Mkoa Ukitafuta namna ya Kusaidia Wanafunzi Kuendelea na Mafunzo baada ya kufunguliwa kwa Shule hiyo kesho Julai 11, 2016
Aidha, Mkuu wa Mkoa amewashukuru wananchi wote waliojitokeza kuuzima moto huo kwani haikuwa kazi rahisi, pia amewashukuru Polisi na Jeshi la zimamoto kwa jitihada walizochukua katika kuudhibiti moto huo.
Kwa sasa inafanyika tathmini ya mali zilizoteketea kutokana na moto huo sambamba na uchunguzi wa chanzo cha moto. Taarifa kamili ya uchunguzi na tathmini itatolewa pindi itakapokamilika.
Katika hatua nyingine mtu mmoja alietaka kuiba Komputa mpakato katika tukio hilo amekamtwa na Polisi Baada ya Wananchi kuanza kumpa adhabu.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoani Lindi, wakiendelea na jitihada za kuuzima moto huo.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi (kushoto) akiwa anashauriana jambo na baadhi ya wajumbe waliofika kuzima moto.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika kuuzima moto huo katika Shule ya Sekondari ya Lindi.
Jengo la Maabara ambalo limeungua paa tu, lakini ndani moto haukufika.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mhe. Godfrey Zambi (aliyevaa kofia) akiwashukuru wananchi waliojitokeza kuuzima moto huo pamoja na vyombo vya Ulinzi na Usalama na Zimamoto. Majengo ya yanayoonekana kwa nyuma ni madarasa yaliyoungua na moto.
Sehemu ya Majengo yaliyoungua moto.
Baadhi ya vitu vilivyookolewa katika tukio hilo la Moto.
No comments:
Post a Comment