Thursday, 7 July 2016

AFRIKA:Watu 9 wauawa katika sherehe ya Eid Ghana



Watu tisa (9) wameuwawa katika mkanyagano wakati wa kusherekea sikukuu ya kiislamu ya Eid Ul- fitr inayoadhimishwa kumalizika kwa mfungo wa mwenzi mtukufu wa Ramdhani,hajabainika wazi haswa kilichosababishwa mkanyagano huo katika mji wa Kumasi kuna taarifa za kutatanisha ya sababu ya kukanyagana Jumatano usiku.Vyombo vya habari nchini humo vinaripoti kwamba kulizuka vita wakati wa sherehe za maadhimisho hayo na wakati watu walijaribu kutoroka ndipo hapo mkanyagano ulipotikea,Wengine wanasema nguvu za umeme zilipotea kwa kishindo kikubwa sawa na risasi iliyofyatuliwa na kusababishwa hali ya taharuki.


Vile vile inadaiwa kuwa na milango ya ukumbi huo ilikuwa imefungwa na hivyo kusababisha maafa hayo yaliyotokea,Watu kadhaa wamejeuriwa na wanatibiwa hospitali,waliokufa ni wanawake sita (6) na wanaume watau(3)

No comments:

Post a Comment