Friday, 15 July 2016

NEW PANGANI IN COAST:UJENZI WA KIVUKO KIPYA CHA MV PANGANI KUKAMILIKA JULAI MWAKA HUU.

 kutoka ni Mtendaji Mkuu TEMESA Mhandisi Lekujan Manase (wa kwanza kushoto) akioneshwa moja ya mtambo wa kuendeshea kivuko (propulsion unit) alipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko kipya cha Mv Pangani unaofanyika katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam.
 Kivuko kipya cha Mv Pangani katika hatua za kukamilika kwa ujenzi wake, unaofanyika katika eneo la Bandari ya Dar es salaam.Picha zote na Theresia Mwami,TEMESA.

Na Theresia Mwami - TEMESA.
Ujenzi wa kivuko kipya cha Mv Pangani uko katika hatua za mwisho na kinategemea kumamilika Julai mwaka huu na  kuanza kutoa huduma.

Hayo yamesemwa na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi. Lekujan Manase alipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa kivuko hicho ambao upo mbioni kukamilika kwa kuanza kutoa huduma kwa wananchi.

“Kivuko hiki kipo katika hatua za mwisho za ujenzi wake na leo tumekuja hapa kukagua mitambo ya kuendeshea kivuko (propulsion units) pamoja na injini zilizofungwa katika kivuko hiki ili kukamilisha ujenzi wake na hatimaye kianze kufanya kazi” alisema  Mhandisi Manase.

Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka Idara ya Huduma za Ufundi na Umeme kutoka Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Dkt. William Nshama alieleza kuwa ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa kivuko hicho unaofanywa kwa kiwango cha kimataifa na kuwa kivuko cha Mv Pangani kinatarajiwa kutoa huduma kati ya Pangani na Bweni Mkoani Tanga baada ya ujenzi wake kukamilika.

Kwa mujibu wa kampuni ya Songoro Marine Transport LTD kivuko hicho kina uwezo wa kubeba magari sita na abiria 100 kwa pamoja, na ni sawa na uzito wa tani 50.

No comments:

Post a Comment