Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu akisalimiana na watumishi wa kituo hicho cha afya.
Waziri wa afya akuongea na wagonjwa walifiks kituoni hapo kupata huduma(picha na Habari na wizara ya afya.
Mmoja wa watumishi wa kituo hicho akimsomea taarifa ya kituo hicho cha afya waziri wa afya(hayupo pichani).
………………………………………………………………………
Na.Mwandishi wetu,Bahi
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, Ummy Mwalimu amewahimiza wananchi wa wilaya ya Bahi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya.
Waziri Ummy alisema hayo leo wakati alipofanya ziara ya kikazi wilayani BAHI ambapo kwa kutembelea kituo cha Afya cha Mundemu.
Akijibu maswali ya wananchi kuhusu kutopewa dawa licha ya wao kuwa na kadi za CHF, Waziri Ummy amewahakikishia wananchi wote kuwa, wizara yake kupitia Bohari ya Dawa(MSD) itahakikisha dawa za kutosha zinapatikana kwenye vituo vya kutolea huduma ili wananchi na wanachama wa CHF waweze kupata dawa wakati wote.”kupitia CHF iliyoboreshwa mtaweza kupata huduma hizo hadi ngazi ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa”alisema
Katika ziara hilo,Waziri Ummy pia alitembelea mradi wa usafi wa mazingira mashuleni, katika jamii na maeneo ya kutolea huduma kwa jamii unaofadhiliwa na PLAN INTERNATIONAL

No comments:
Post a Comment