Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna
Simon Sirro akizungumza na mashabiki wa Timu ya Yanga kwenye Mchezo uliopita dhidi ya Tp Mazembe uliochezwa Juni 28 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MABINGWA wa Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara na wawakilishi wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika Afrika Mashariko na Kati timu ya Yanga imesema kuwa inahitaji ushindi kwenye mchezo huo na zaidi kocha mkuu wa Yanga Hans Van de Pluijm amesema lazima timu yake itaibuka na ushindi katika mchezo huo ambao ni muhimu kwao.
Amesema, mchezo huo ni muhimu kwao na watahakikisha hawapotezi pointi tatu kwa namna yoyote ile na ushindi katika mchezo dhidi ya Medeama ndio utakaoamua Yanga kusonga mbele au laa.
Katika kuelekea mchezo huo muhimu kwao amewapa mbinu za jinsi ya ushambulia wachezaji wake ili kuhakikisha hawapotezi nafasi wanazozitengeza. "Katika mchezo uliopita wachezaji wangu walitengeneza nafasi nyingi lakini walishindwa kuzitumia ipasavyo na kufanya tupoteze mchezo wetu wa nyumbani", amesema Pluijm.
Kwa upande wake kocha wa Medeama ya Ghana, Prince Yaw Owusu, ametamba kuibuka na ushindi katika mchezo wa leo dhidi ya wapinzani wake.Nawajua vizuri wapinzani wangu hivyo hana wasiwasi na mchezo huo na unasilimia kubwa ya kuondoka na alama tatu. "Nina uzoefu na timu ya Yanga kwani nilishaiona katika michuano ya Kagame nilipokuwa na kikosi cha timu ya Al Khartoum ndio maana nasema nina uhakika wa kushinda mchezo huu", amesema.
Nao shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) limewataka washabiki na wapenzi wa Yanga kuwa watulivu katika mchezo huo. Ni imani yao kama shirikisho kuwa watashangilia timu yao kwa utulivu na amani ili kuhakikisha inapata alama tatu.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna
Simon Sirro amesema kuwa ulinzi utaimarishwa katiika mchezo huo ili kuwa na mvuto.
Wananchi wasiwe na shaka yoyote kwani wamejipanga kuhakikisha usalama unasimamiwa kwa asilimia mia na hawatafumbia macho kitendo chochote cha uvunjifu wa amani.
No comments:
Post a Comment