Sunday, 3 July 2016

MBUNGE WA KIBAMBA JOHN MNYIKA ATOA A MOYONI LEO BAADA YA KIMYA KIREFU



TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI;Mtakumbuka ni muda sasa sijaonekana katika harakati za kisiasa,Leo nimependa kuweka bayana ili umma wa watanzania ufahamu kwani kumekuwa na upotoshaji wa mkubwa juu ya ukimya wangu
Napenda umma wa watanzania ufahamu yafatayo;
1.Msimamo wangu wa kuitaka serikali imkamate Mh.Edward Lowasa imhoji na imchukulie hatua kwa mujibu wa sheria kutokana na ushiriki wake katika kashfa ya RICHMOND haujabadilika kama nilivyowahi kusema nikiwa mkurugenzi wa vijana wa CHADEMA tarehe 25 february 2008 na kipindi chote nikiwa mbunge wa ubungo
Hivyo nategemea kuanzishwa kwa mahakama ya mafisadi Lowasa ndiyo atakuwa wa kwanza siwezi kusaliti msimamo wangu bora nipotezee ubunge wangu
2.Sikubaliani na utaratibu uliotumika kumpata mgombea wa urais ndani ya chama changu hususani ujio wa Mh. Edward Lowasa mmoja wa watu ambao ni mzizi wa ufisadi hapa nchini,Hai hii ilinilazimu nikae kimya kutokana na kutoamini kilichokuwa kinatokea hususani kwa chama changu cha CHADEMA kilichojijenga na kujipatia umaarufu kwa kuongoza mapambano dhidi ya rushwa,ubadhilifu,ufisadi na uwajibikaji mbovu wa serikali  halafu tukasaliti msimamo wetu kwa uharaka wa kupata dola!Sikubaliani na sijakubaliana nalo hata sasa
3.Napenda kuzungumzia utendaji wa serikali ya Dkt.Magufuli naomba ifahamike nimekuwa mara zote nikisema matatizo ya ya nchi yetu hayasababishwi na mapungufu ya  sheria ila kwa kiasi kikubwa uchangiwa na kulegea kwa misingi ya utawala wa sheria na uwajibikaji miongoni mwa viongonzi.Hivyo kwa asilimia kubwa naona Dkt. Magufuli ameweza kujibu niichokuwa nikikilaamikia kwa muda mrefu sasa.Haya mengine yanazungumzika
4.Sikubaliani na mtazamo wa baadhi ya viongonzi wakiwemo wa chama changu wanaotaka fedha za walipa kodi ziendeee kuteketea kwa ufisadi na ubadhilifu huku wahusika ambao wachache wakiindwa kwa kisingizio cha haki za binadamu.Kwa hii nampongeza Mh. Rais kwa misimamo na hatua anazochukua japo apanue wigo ii watanzania maskini wanufaike na utajiri wa rasiimai waizojaiwa
5.Vilevile naomba kuzungumzia mwenendo wetu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni au UKAWA binafsi sifurahishwi na maagizo na maeekezo ya viongonzi wetu juu ya kuingia na kutoka bungeni kwa hoja ambazo haziwagusi moja kwa moja kiasi cha kufanya tushindwe kutimiza majukumu yetu kama wabunge kwa mujibu wa ibara ya 63(2) na (3) katiba ya jamhuri ya muungano ya Tanzania ya kutunga sheria,kusimamia serikali,kuwawakiisha wananchi na kupitisha mipango ya maendeleo.Sifurahishwi sababu kutoka  kwetu hakuna a msingi tunaoifanya kwa ajili ya wananchi waiotutuma huko bungeni.Tusipoangaia itatugharimu
Mwisho nawatakia waumini wote wa kiisamu mfungo mwema wa mwenzi mtukufu wa Ramadhani.
Imetoewa tarehe 03/07/16
John Mnyika(mb)
0754694553

No comments:

Post a Comment