Tuesday, 19 July 2016

NEW MUFINDI IN IRINGA:MKURUGENZI MTENDAJI WA HALMASHAURI YA MUFINDI DKT. RIZIKI SHEMDOE AKAGUA UPOKEAJI WA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO

Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Dkt. Riziki Shemdoe (katikati wa nne) akikagua upokeaji wa wanafunzi wa kidato cha tano katika shule ya sekondari mdabulo katika iliyoko Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa. Shule hiyo ambayo iko umbali wa km 45 kutoka mji wa Mafinga upande wa mashariki mwaka huu imeanza kufundisha  programu za masomo ya kidato cha tano na sita katika mchepuo wa Sanaa HGK,HKL na HGL.
Baadhi ya wanafuzi wa shule ya sekondari mdabulo iliyoko wilayani Mafinga mkoa wa Iringa wakipata huduma ya maji safi katika eneo la shule hiyo ambayo ni ya mchanganyiko wa wavulana na wasichana kwa “O – Level” na wasichana pekee kwa “A – Level”. 
Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Dkt. Riziki Shemdoe (kushoto) akikagua uwepo wa madawati katika madarasa ya shule hiyo ambayo kwa mara ya kwanza imeanza kufundisha programu za masomo ya kidato cha tano na sita katika mchepuo wa Sanaa.
MkurugenziMtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Dkt. Riziki Shemdoe
(katikati) akikagua mazingira na miundombinu ya shule hiyo akiwa ameambatana na
viongozi wa shule hiyo.

No comments:

Post a Comment