Friday, 8 July 2016

WAFANYAKAZI WA NGAZI YA ZAHANATI WANAONGOZA KWA KUDUMU KATIKA VITUO VYAO VYA KAZI- DK ELLEN.

WAFANYAKAZI wa ngazi ya zahanati wanaoongoza kubaki katika vituo vya vya kazi kuliko wa ngazi zingine zote

Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro wakati akizungumza wadau wa afya wa kutoka mkoa Mbalimbali hapa nchini katika warsha kuwasilisha matokeo ya Tathmini mbalimba za Rasilimali watu katika sekta ya Afya zilizofanywa na taasisi ya Benjamini Mkapa leo jijini Dar es Salaam leo.

amesema kuwa Taasisi ya Mkapa imetoa matokeo ya Tathmini za rasilimali watu ambazo zimefanywa katika sekta ya afya katika Halmashauri 17 za Wilaya zilizopo mikoa 7 ya Tanzania Bara.  

Dk. Ellen  amesema kuwa  Sababu zinachangia kubaki kwenye vitu vyao kazi ni pamoja na Kupewa motisha ya posho ya kujikimu na nyumba ya kuishi karibu na vituo vyao, Kupewa ardhi kwa gharama nafuu ikiwa na viongozi wa halmashauri wanawasaidia watumishi wa Afya kujiwekea malengo ya utendaji kazi wao.

Hata hivyo Dk. Ellen ameomba Mfumo wa OPRAS ufanyiwe meboresho ili uendane na baadhi ya kada katika sekta ya Afya. 

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro akizungumza na wadau wa afya wa kutoka mkoa Mbalimbali hapa nchini katika warsha ya kuwasilisha matokeo ya Tathmini mbalimba za Rasilimali watu katika sekta ya Afya zilizofanywa na taasisi ya Benjamini Mkapa leo jijini Dar es Salaam.
 Mwakilishi wa shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani( UNFPA) hapa nchini, Dk. Natalia Kanem akizungumza na wadau wa afya katika warsha ya kuwasilisha matokeo ya Tathmini mbalimba za Rasilimali watu katika sekta ya Afya zilizofanywa na taasisi ya Benjamini Mkapa leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Mradi na Msimamizi wa Sera na Utetezi wa Taasisi ya Mkapa, Manka Kway akizungumza katika warsha ya kuwasilisha matokeo ya Tathmini mbalimba za Rasilimali watu katika sekta ya Afya zilizofanywa na taasisi ya Benjamini Mkapa leo jijini Dar es Salaam.





 Baadhi ya wadau wa afya Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mkapa, Dk. Ellen Mkondya Senkoro katika warsha ya kuwasilisha matokeo ya Tathmini mbalimba za Rasilimali watu katika sekta ya Afya zilizofanywa na taasisi ya Benjamini Mkapa leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment