Tuesday, 5 July 2016

BIASHARA:WAZIRI WA AJIRA, VIJANA ATEMBELEA BANDA LA LAPF KATIKA MAONYESHO YA 40 YA BIASHARA YA KIMATAIFA

L1Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akipata maelezo ya ujumla kuhusu Mfuko wa Pensheni wa LAPF katika maonyesho ya 40 ya biashara ya kimataifa. Anayetoa maelezo ni Afisa Masoko Mwandamizi wa Mfuko Bi. Rehema Mkamba.
L2Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akipata maelezo kutoka kwa Afisa wa Mifumo ya Kompyta wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bw. Yohana Nyabili kuhusu upatikanaji wa taarifa za michango ya wanachama kupitia tovuti ya Mfuko www.lapf.or.tz na simu za viganjani kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini Dar es Salaam.
L3Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akionyeshwa taarifa yake ya michango ya Hiari LAPF kwenye maonyesho ya biashara ya 40 ya kimataifa jijini DSM. Anayemhudumia ni Afisa Mafao ya Mfuko wa Pensheni wa LAPF Bi. Irene Michael.
L4Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Ajira, Vijana, Wazee na Wenye Ulemavu Mh. Jenista Mhagama (Mb) akipata maelezo kuhusu shughuli za uwekezaji za Mfuko wa Pensheni wa LAPF pamoja na mipango ya Mfuko kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2016/17, anayetoa maelezo ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Mfuko Bw. James Mlowe.
L5Baadhi ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF kutoka Jeshi la Polisi wakipata maelezo mbalimbali ya Mfuko kutoka kwa Afisa wa Mfuko Bw. Yohana Nyabili kwenye maonyesho ya biashara ya kimataifa ya 40 yanayoendelea jijini DSM.
L6Wanachama na wadau mbalimbali wa Mfuko wa Pensheni wa LAPF wakipata maelezo mbalimbali kuhusu manufaa na huduma za Mfuko ikiwemo utaratibu wa kujiunga na kuweka akiba kwa hiari kwenye Mfuko. Anayetoa maelezo ni Afisa mafao wa Mfuko Bi. Judith Lupondo.

No comments:

Post a Comment