Friday, 15 July 2016

NEW RUANGWE IN MBEYA:MAKALLA AFANIKISHA KUANZA KWA UJENZI WA KITUO CHA AFYA CHA MPUGUSO-RUNGWE,AFANIKISHA MSAADA WA MIFUKO 150 TOKA MBEYA CEMENT.

   
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla Leo katika kata ya Mpuguso Kijiji Cha Mpuguso Wilaya Ya Rungwe ametembelea Ujenzi wa Kituo Cha Afya Cha Mpuguso unaondelea katika Kata hiyo Kwa kushirikisha nguvu za Wananchi , wadau pamoja na Serikali. 
Akizungumza na wananchi Mh.Rc.Makalla ameahidi kutoa ushirikiano Mpaka kukamilika Kwa Kituo Cha Afya Cha Mpuguso, 
alisema "nimekubali kuwa Mlezi wenu wa Kimaendeleo katika kila hatua ya Ujenzi mtakapokwama mnijulishe tutafanikiwa"
Pia Makalla amewashukuru Mbeya Cement Kwa kukubali Ombi lake la Msaada wa Saruji (Cement ) Kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo hicho, Mbeya Cement wamemkabidhi Mifuko ya Cement 150 Kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo hicho. 
Makalla amewataka wanasiasa kutokuingiza Siasa katika Masuala ya Kimaendeleo kwani hayana tija Kwa ustawi wa Maendeleo ya wananchi wa hali ya chini wanyonge. Ameahidi kushirikisha wadau katika kukamilika Ujenzi haraka wa Kituo Cha Afya , Mwishoni katika Salamu za wananchi Wamemuomba Mh.Rais Dkt.John Magufuli kutokumwamisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla kwani ni Kimbilio la wanyonge, tangu amewasili Mkoa wa Mbeya 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh.Amos Makalla Akiwasili katika kata ya Mpuguso Kijiji Cha Mpuguso Wilayani Rungwe.
Mkuu wa mkoa wa mbeya Mh.Amos Makalla akipokea Mifuko ya Cement 150 Kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo hicho kutoka Mbeya Cement
Mkuu wa mkoa akizungumza na baadhi ya wanakijiji wa  Mpuguso Wilaya Ya Rungwe leo.
PICHA NA JAMES MWAKIBINGA MBEYA.

No comments:

Post a Comment