Saturday, 9 July 2016

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA AKUTANA NA MKUU WA JESHI LA POLISI WA MALAWI DAR ES SALAAM

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akimfafanulia jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama (kulia) wakati wa ziara yake nchini pamoja na ujumbe alioambatana nao walipokutana na Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali ya kupambana na uhalifu. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama (kulia) alipokuwa akimfafanulia jambo kuhusu masuala mbalimbali ya kupambana na uhalifu. IGP Kachama na ujumbe wake yupo nchini kwa ajili ya ziara ya kikazi. Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Waziri Mwigulu, jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (kulia) akimuaga Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Malawi, IGP Lesten Shame Kachama mara baada ya mazungumzo yao ofisini kwake jijini Dar es Salaam. IGP Kachama yupo nchini kwa ziara ya kikazi. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment