Wednesday, 20 July 2016

NEW RELIGION CONGRESSES:MWIGULU NCHEMBA ASHIRIKI KONGAMANO LA VIONGOZI WA DINI

p1Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (wapili kulia) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Baraza la Kuu la Waislamu (BAKWATA), Suleman Said Lolila wakati Waziri huyo alipokuwa anawasili katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam, kwa ajili ya kushiriki Kongamano la Viongozi wa Dini lililojadili masuala ya ugaidi. Kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba, na wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Leonard Mtaita.
p2Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba akizungumza na viongozi wa dini kuhusu masuala mbalimbali ya amani nchini katika Kongamano la Viongozi wa Dini lililofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es salaam. Katika hotuba yake, Waziri Mwigulu aliwataka viongozi hao kutokuhusisha kosa lifanyalo na mtu au watu fulani kulifananisha na dini yake, amewaomba viongozi hao watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa za matukio mbalimbali ya kiuhalifu nchini. Kutoka kulia ni Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Paul Ruzoka, Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeiry Bin Ally na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Leonard Mtaita.
p3Sehemu ya viongozi wa dini walihudhuria katika Kongamano la Viongozi wa Dini nchini lililofanyika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo ambalo lilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (hayupo pichani), lilijadili masuala mbalimbali ya ugaidi pamoja na ushirikiano wa dini mbalimbali nchini. Hata hivyo Waziri Mwigulu aliwataka viongozi hao kutokuhusisha kosa lifanyalo na mtu au watu fulani kulifananisha na dini yake, amewaomba viongozi hao watoe ushirikiano kwa kutoa taarifa za matukio mbalimbali ya kiuhalifu nchini.
p4Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (watatu kulia) akiandika maelezo ya hotuba ya Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Dk Leonard Mtaita (kushoto) katika kongamano la viongozi wa dini lililofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kongamano hilo lilijadili kuhusu ugaidi na ushirikiano wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT Mstaafu, Alex Malasusa. Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeiry Bin Ally (wapili kushoto), Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Tabora, Paul Ruzoka (watatu kushoto) na Mufti wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omar.
p6Mkurugenzi wa Idara ya Sheria wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Marlin Komba akimfafanulia jambo Mufti Mkuu wa Tanzania, Abubakary Zubeiry Bin Ally (kushoto) mara baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu M.L Nchemba (hayupo pichani) kuzungumza na viongozi wa dini kuhusu masuala mbalimbali ya amani nchini katika Kongamano la Viongozi wa Dini lililofanyika katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Sheria wa Wizara hiyo, Berious Nyasebwa

No comments:

Post a Comment